2012-10-12 15:40:27

Maeneo ya Makaburi ya Wakristu yaharibiwa Dakar - Senegal


Jiji la Dakar limeshitushwa na kitendo cha kinyama cha kuharibu makaburi zaidi ya 160 katika maeneo mawili ya Makaburi ya Wakristu ya mjini Dakar, uovu uliofanywa usiku wa tarehe 6 kuamkia 7 Ocotba 2012 , mjini Dakar Senegal
.
Gazeti mahalia L’Observateur, limenukuliwa na Apic , likieleza kwamba, katiak shambulio hilo, misalaba iliyokuwa katika makaburi iling’olewa na baadhi ya vitu vilivyokuwa vimewekwa makaburini kuibiwa.

Kanisa mahalia limekemea vikali kitendo hiki likisema ni unyama usioweza kukubaliwa na watu waliostraabika , na ni udharirishaji wa maeneo nyeti kama makaburi, kinyume pia na utamaduni wa Wasenegal , ambao daima huheshimu makaburi na marehemu.

Na Askofu Mkuu Theodore Kardinali Adrien Sarr na Tume ya inayoshughulika na maeno ya makaburi ya Wakristu katika jiji la Dakar , wamesema, Misalaba ni alama kuu ya Imani ya Wakristu , na hivyo Kitendo chochote cha kuchezea au kuharibu msalaba ni kufuru. Kardinali Sarr, amewahimiza waamini na wasiokuwa waamini kuongoeza juhudi zao katika ujenzi wa mshikamano na umoja kama hatua ya kuzimisha moto wa uchokozi na uchochezi unaofanywa kichinichini na watu wasiolitakia mema taifa la Senegal.

Kanisa pia limeiomba serikali kwa wakati huu kuongeza ulinzi makaburini iwe ya Wakristu au Waislamu, kama hakikisho la kuheshimu maeneo hayo na Marehemu waliozikwa humo.








All the contents on this site are copyrighted ©.