2012-10-11 07:53:03

Sinodi- Hotuba ya Askofu Mkuu Rino Fisichella


Askofu Mkuu Rino Fisichella, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji mpya, Jumannne hii akiwa Mwenyekiti wa sinodi, aliwaangalisha wajumbe , juu ya umuhimu wa mwanzo wa mwaka wa Imani , kuzinduliwa sanjari na adhimisho la miaka 50 ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican Baraza.

Amesema, kuenda sambamba kwa matukio haya, imekuwa ni nafasi nzuri ya kupatanisha utendaji wa kanisa kwa nyakati hizi..

Na katika mwanga wa mastahili haya yayokwenda sambamba na uzinduzi wa Mwaka wa Imani,inaonyesha dhahiri, ishara wazi ya mafanikio ya Mtaguso Mkuu wa pili wa Vatican.
Askofu Mkuu metoa wito kwa waamini katika kipindi hiki cha kufunguliwa kwa mwaka wa Imani , kujiandaa vyema kwa ajili ya Ibada ya Ekaristi Takatifu, pia kusoma nyaraka za Mtaguso, na kufanywa upya maisha ya Kanisa, ili wapate mastahili bora ya kiroho. Amesema ni wakati wa kurejea tena maadilaino ya muda mrefu ya Oktoba 1962, ambamo Maaskofu walijumuika , kama walivyoongozwa na Baba Mtakatifu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu.
Miaka hupita, lakini utendaji wa kanisa unabaki na umuhimu huohuo wa kuihubiri Injili ya Kristo. Na hiyo ni sababu kuu kwa Wakristu kufurahia utume huo, wakijisikia kuwa sehemu ya kanisa.







All the contents on this site are copyrighted ©.