2012-10-09 15:39:52

Uinjilishaji mpya unapaswa kusimikwa katika mizizi ya makopokeo ya Kanisa-Kardinal Wuerl


Juhudi Katoliki za kuwafikia waamini wanaosinzia nje ya kanisa, ni muhimu zikaonyesha umuhimu wa imani leo hii. Na inapaswa kufanyika hivyo, bila ya kupoteza mapokeo msingi na utambulisho wa imani Katoliki. Kardinali Donald W. Wuerl wa Jimbo Kuu la Washington, alisema mbele ya Papa Benedict XVI na Mababa wa Sinodi inayoendelea hapa Vatican.

Kardinali Wuerl, ni kati ya walioteuliwa na Papa, kutoa maelezo ya awali , katika kazi za Sinodi, kwenye mtazamo mpana wa kimataifa juu ya changamoto za leo katika uinjilishaji, na maadili yanayotakiwa kama msingi wa kanisa , katika kuwafikia watu.

Kardinali alisema " tsunami" hii ya malimwengu, imekumba kote, na kuacha watu na tabia ya ukana Mungu, au kuukataa ukweli kwamba, uwepo wa Mungu ni muhimu katika kufikiri na utendaji kote kwa binadamu. Na Kazi ya Uinjilishaji mpya ni kuwasaidia watu kuona kwamba utu na haki za binadamu ni mtiririko kutoka ukweli kwamba , binadamu wameumbwa kwa mfano wa Mungu.

"Uinjilishaji mpya lazima kuzungumzia upendo wa Mungu wa kuokoa kwa watu wote na, wakati huo huo, kutambua kwamba Yesu, ametoa njia ya wazi na ya kipekee ya ukombozi na wokovu," alisema Kardinali.

Mafundisho ya kanisa, aliendelea, huthibitisha ukweli wa kile kinachohubiriwa na watu wakati wakijaribu kushirikishana Injili na wengine na kanisa ni njia ambayo Mungu husambaza neema zake, hasa kupitai njia za sakramenti.

Kardinali Wuerl aliwaambia wajumbe wa sinodi, kwamba, katika muda huu wa wiki tatu , wataweza kuangalia kw aukaribu zaidi kila ya maisha ya kanisa na katika fursa mbalimbali, na pia vikwazo vya uinjilishaji mpya. Hivyo kazi yao itakuwa ya kujibu kwa "ujasiriā€, mshikamano wa kanisa, katika maana ya dharura na furaha. "

"Kanisa daima linaitwa kwanza kujitafakari lenyewe . Na kila muumini wake, anapaswa kujiuliza kama anaiisha imani yake kikamilifu kila siku. Na si swala la maneno lakini kiutendaji.








All the contents on this site are copyrighted ©.