Papa aongoza Ibada ya Misa kwa ajili ya kufungua Sinodi juu ya Uinjilishaji Mpya.
Jumapili hii majira ya asubuhi , Mkutano wa Sinodi ya 13 ya kawaida ya Maaskofu, utakaochukua
muda wa wiki tatu hapa Vatican 7-28 Octoba 2012, umefunguliwa na Baba Mtakatifu Benedikto
XV1, kwa Ibada ya Misa, iliyofanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.
Ibada ilitanguliwa na sala ya Rosare Takatifu ikisindikizwa na nyimbo za
kwaya na maelezo kadhaa ya juu ya mawazo ya Mtakatifu Yohane wa Avila na Mtakatifu
Hildegard Bingen waliotajwa kuwa walimu wa Kanisa. Na mwisho wa Rosare kengere zilipigwa,
na kutokea mbele ya lango kuu la Kanisa la Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu aliingia
kwa maandamano akitanguliwa na Makardinali, Mapatriaki wajumbe wa sinodi, na Maaskofu,
kwa ajili ya kuanza Ibada ya Misa.
Baba Mtakatifu, katika mahubiri yake
, alilenga zaidi katika mada itakayoongoza Sinodi: Uinjilishaji mpya kwa ajili ya
Uenezaji wa Imani ya Kikristu . Alisema mada hii inatazamisha katika mwelekeo wa kimipango
kwa maisha ya kanisa , waamini familia , jumuiya na taasisi zake. Mipango inayoleta
msukumo wa kufanyika sanjari na kuanza kwa Mwaka wa Imani, hapo tarehe 11 Oktoba
2012, ikienda sambamba na maadhimisho ya miaka hamsini kupita, tangu kuzinduliwa kwa
Baraza Pili la Kiekumeni la Vatican, Octoba 1962.
Papa aliwakaribisha na
kuwashukuru wajumbe wote wa Sinodi hii aliyoizindua, na kutoa mwaliko kwa waumini
, katika muda huu wa wiki tatu zijazo , waisindikize Sinodi kwa sala.
Na
akirejea masomo ya Liturujia yaliyosomwa, aliainisha ujumbe wa masomo hayo kwamba,
mna vipengere viwili, kwanza ni juu ya ndoa, na jambo la pili ni juu ya Yesu Kristu,
Neno wa Mungu, Mtukufu sana, aliyesulubiwa ili wote wapate kuwa na uzima. Hvyo, kwa
namna ya kipekee, sinodi hii, itafanyika katika kumtazama sana Yeye katika mwanga
wa fumbo lake.
Katika vipindi vyote vya nyakati na mahali, Uinjlishaji daima
umekuwa ni juu ya mwanzo wake na mwisho wake, Yesu Kristu Mwana wa Mungu. Na Msalaba
ni ishara maalum inayomtambulisha, Yeye anayetajwa katika Injili ; Ishara ya upendo
na amani , mwaliko wa uongofu na upatanisho.
Papa kwa maelezo hayo aliwaalika
ndugu zake Maaskofu, waanze wao wenyewe kutakatifusha dhamiri zao kwa neema yake.
Papa
kwa kifupi, alitafakari juu uinjilishaji mpya, na uhusiano wake na uinjilishaji wa
kawaida na kwa mataifa. Alisema, Kanisa lipo kwa ajili ya kuinjilisha. Wanafunzi wa
kwanza wa Bwana Yesu Kristo, walitii amri ya mwalimu wao na walikwenda nje , dunia
nzima kuitangaza Habari Njema, kueneza jumuiya za Kikristo kila mahali, kama historia
ya uinjilishaji inayoonyesha katika vipindi vyote ,wakati watu wa Anglo-Saxon au
Slavs, huko Amerika, kazi za misioni Afrika, Asia na Oceania.
Kwa namna hiyo,
hata katika nyakati zetu wenyewe, Roho Mtakatifu anaendelea kuwa ndani ya kanisa,
akitoa nguvu mpya kwa waamini, kwenda nje na kuihubiri I njili, kulingana na mabadiliko
ya nyakati , kama ilivyo elezwa katika waraka wa Mtaguso Mkuu wa pili wa Vatican.
Kiinjili, upya huu wa mabadiliko, huzalisha ushawishi kifadhili , kwa namna mbili
maalum, kwamba, kwa upande mmoja, ni Utume kwa mataifa, wa kutangaza Injili kwa
wale ambao hawana bado kumjua Yesu Kristo na ujumbe wake wa wokovu, na kwa upande
mwingine ni Uinjilishaji Mpya, unaoongoza kwa wale ambao, ingawa wamebatizwa, wamejitenga
mbali na kanisa au sasa wanaishi nje ya maisha ya Kikristu.
Hivyo Papa alisema,
Kikao cha Sinodi iliyofunguliwa, inakuwa ni majitolea kwa uinjilishaji mpya, kusaidia
watu watu kukutana na Bwana, ambaye peke ndiye ukamilifu wa maisha na amani; kuigundua
imani, kwamba ni chanzo cha neema ambayo huleta furaha na matumaini kwa maisha ya
mtu binafsi, familia na jamii kwa ujumla.
Papa ameweka bayana kwamba, ni wazi
lengo hili maalum, halipunguzi juhudi za kimisionari katika utendaji wake au shughuli
za kawaida za uinjilishaji katika jamii yetu ya Kikristo.