2012-10-08 09:45:44

Mwizi wa nyaraka za Papa ala kifungo cha miezi18 jela


Mahakama ya Vatican, Jumamosi ilitoa hukumu ya kifungo cha miezi 18 jela kwa Paulo Gariel , baada ya kumwona ana hatia katika kesi iliyomkabili ya kuiba na kusambaza nyaraka binafsi za Papa na Vatican bila idhini kwa wanahabari.

Paulo Gabriel, alitenda makosa hayo wakati akilitumikia Kanisa, kwa cheo cha msaidizi wa karibu wa Papa Benedikto XV1. Na alikamatwa May 23, 2012 na vyombo vya usalama vya Vatican , kufuatia tatizo la uvujaji wa taarifa, kutoka ndani ya vatican.

Jumamosi 6 Octoba 2012 , Jopo la Majaji watatu walio sikiliza kesi hii, iliyoanza kusikilizwa 29 Septemba 2012, wakiongozwa na Rais wa jopo hilio, Giuseppe Dalla Torre, walisoma hukumu hiyo kwa mshitakiwa na Maneno; Kwa niaba ya Baba Mtakatifu Benedikto XV1, , Mtawala Mtukufu, Mahakama ikiongozwa na Utatu Mtakatifu , inatoa adhabu ya kifungo cha miezi 18 jela kwa mtuhumiwa Paulo Gabriel. .

Na kwamba majaji wamemwona Gabriel, kuwa na makosa yanayostahili kifungo cha miaka mitatu, lakini adhabu hiyo imepunguzwa kwa misingi minne kwamba, Gabriel kabla, alikuwa hajashitakiwa mahakamani kwa uhalifu, pia mahakama imethamini miaka aliyotumikia Vatican bila makosa, na utetezi wake kwamba, ametenda makosa haya akiwa ameshawishika kwamba ana nia jema kwa kanisa na pia kwa yeye kutambua kwamba alikuwa akisaliti uaminifu wake kwa Papa.

Usomaji wa hukumu hii ulichukua muda wa dakika tano na Gabriel hakuonyesha kushtuka wakati hukumu inasomwa. Na mara alichukuliwa na Polisi .

Mwana sheria wake mtetezi , Christiana Arru , alionyesha kuridhika na hukumu iliyotolewa akisema, kuna urari . Na bado mteja wake alikuwa hajaamua kama anataka kukata rufaa. Mahakama imetoa muda wa siku tatu wa kukata rufaa kama anataka.

Msemaji wa Vatican, Padre Federizo Lombardi , nae aliwaambia wanahabari kwamba, Papa alipewa taarifa za hukumu hiyo mara na anafuatilia. Na kuna mwelekeo wa kumsamehe, ingawa haijulikani lini.








All the contents on this site are copyrighted ©.