Tujali matendo kuliko maneno -Hayati Kardinali Laurian Rugambwa.
Maelfu ya waumini wa Kanisa Katoliki kutoka ndani na nje ya nchi, walifurika kwa
wingi mjini Bukoba kuhudhuria mazishi ya Kardinali wa kwanza Mwafrika, hayati Kardinali
Laurian Rugambwa aliyefariki takriban miaka 15 iliyopita, kama tulivyokuwa tayari
tunawelezea katika habari zetu na makala zetu. Itakumbukwa kwamba Kardinali Rugambwa
alikuwa mpenzi mkubwa wa mama Bikira Maria na ambaye kikanisa aliiweka Tanzania chini
ya usimamizi na mwombezi wa Bikira Maria siku moja kabla ya uhuru wa Tanganyika hapo
Desemba nane, na mwezi kama huu mwaka 1997 Kardinali allitwa katika makao ya Bwana
kwa pumziko la milele. Mazishi haya yaliyovuta watu wengine wakiwemo wa madhehebu
mbalimbali ya kidini kwani ikumbukwe kuwa tukio hili linaenda sambamba na maadhimisho
ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa Kardinali huyo pamoja na sherehe za kutabaruku Kanisa
Kuu ambalo limekarabatiwa upya chini ya msimamizi wa ‘’Bikira Maria mama wa huruma’’,
hivyo ni matukio matatu kwa wakati mmoja ambayo yamefikia kilele katika mwezi wa Bikira
Maria. Taarifa kutoka vyombo vya habari na hasa tulivyoweza kuongea navyo moja
kwa moja ni Radio Maria tulielezwa kuwa mitaa yote ilijaa watu katika nyumba zote
za kulala wageni, seminari na sehemu nyingine katika familia mbalimbali hili watu
wapate kuudhuria tukio hili la kihistoria;Ndugu wapenzi hata katika usalama, hali
ya ulinzi iliimarishwa zaidi kuhakikisha utulivu wa mji, hili shughuli za kiroho ziweze
kwenda vizuri. Ibada ya misa iliyanza majira ya saa 5.30 huko Parokia ya Kashozi,
iliudhuriwa na maelfu ya watu maaskofu, mapadre, watawa, viongozi mbalimbali wa serikali,
wageni kutoka nchi jirani na waamini. Askofu Mkuu wa Jimbo la Mwanza Mwashamu Tadeus
Rwahichi aliongoza ibada ya misa . Ndugu wasilizaji wa Radio Vatikan, tukirudi
katika kichwa chetu cha makala yetu ‘tujali matendo kuliko maneno’’ Matendo ndiyo
tunaweza kusema ulikuwa moyo wa hayati Rugambwa kwani mengi yamesemwa na mengi yameandikwa
kuhusu hayati Rugambwa na hasa katika historia yake,wakati huu ni mwafaka kwetu sisi
kuangalia matendo yake, kama wahenga wetu wasemavyo matendo ukidhi aja kuliko maneno,
ambayo hata Askofu Tadeus Rwahichi katika omilia yake alisema si katika ‘’porojo au
mbwembwe’’. Kiongozi huyu alitumia uongozi wake kiroho kwa kujali utu wa mwanadamu
na ndiyo maana alijali matendo zaidi kuliko kutumia maneno, yaani kuthamini umoja
katika madhehebu bila ubaguzi wowote, na kuthamini elimu ya kumpatia maendeleo mtu
kwanza. Taifa lolote linalotaka kuendelea lihaitaji elimu, moyo wa hayati katika
utume ilikuwa ni kitu cha kwanza kuhangaikia wote waliokuwa wako tayari kujitoa bila
kujibakiza, ni mashahidi wa kutosha katika nyanja zote kuanzia, wito mbalimbali wa
mapadre, watawa, madaktari, na watu mbalimbali katika kazi za serikali waliopata msaada
kutoka kwake. Hizo ni juhudi za matendo yake, katika kipaji alichopewa na Mwenyezi
Mungu ambapo tunaweza kusema kweli aliweza kuwatumia watu kiroho na kimwili bila kujali
kabila, muhimu wenye mapenzi mema na kupenda maendeleo. Juhudi zake za kuanzisha
au kuboresha huduma za afya kama hospitali na zahanati mbalimbali ni mojawapo ya huduma
ya kuponya watu mwili na kufariji roho za walio wengi, Kama Yesu mwenyewe alivyofanya
katika utume wake na ndivyo alivyo agiza. Ndugu wikilizaji wa Radio vatikan, hata
Askofu mkuu wa jimbo la Mwanza wakati wa ibada yake ya misa jumamosi parokiani Kashozi
katika kuelezea utume wa Yesu akiunganisha na utume wa hayati katika enjili ya siku
hiyo alionesha kuwa utume wa Yesu ulitekelezwa kwa watu aliokabidhiwa kuwatuliza kiu
yao na kuishi kama watu wa Mungu hili wapate kutulizwa kiu hiyo. Alisema kuwa
enjili kama ingeishia katika aya ya 8 ambayo Filipo alimwambia Yesu kuwa awaonyeshe
baba yao ingetosha,kwamba hiyo ilikuwa sala kubwa ya kutafakari akitumia neno la
kilatini la contemplasio, na kuwa Filipo ni mtangulizi wa hayati Kardinali Rugambwa
katika utume, kama kardinali wa tatu wa Afrika na kama askofu wa kwanza wa Afrika
,alitutangulia kumtamani Mungu, alifundisha siyo porojo au mbwembwe bali alifundisha
Kristo, alifundisha namna ya kumtafuta, kumjua, kumtumikia na kumpenda Kristo. Alifundisha
namna ya kutakatifuza sakramenti za kanisa na alifundisha waliopta fursa ya kumpokea
Mungu, ya kuishi uhai wake Kristo; Aliwatawala kama taifa la Mungu wapate kueneza
ujumbe wa Mungu. Askofu Mkuu aliendelea kufafanua kuwa ni kitendo cha kumshukuru
Mungu kwa yote aliyomjalia ya kumtoa katika kanisa changa hadi kanisa la ulimwengu
, pia kwa vipaji vyake alivyojaliwa akiwa hai, alimwomba Mungu aendelee kuwaita wengi
wenye kujaa ari ya kumtangaza Kristo , na wenye kuwa tayari kabisa kujitoa. Askofu
alielezea ni kwanini Hayati Laurean alihamishwa Parokiani Kashozi alikokuwa amezikwa
kwa muda, kwani kisheria askofu anazikwa mahali alipohudumu, ila kanisa linaruhusu
pia kila askofu kuchagua mahali anapotaka kuzikwa, na hivyo angeweza kuzikwa Dar
Es Salaam lakini pia alihudumia kanisa la Rutabo, na akajenga kanisa la Bukoba, na
upendeleo wake alitaka apumzike mahali pale, na ndiyo maana mapenzi yake yametimizwa. Alielezea
kwamba ni sehemu aliyotumia vizuri ujana wake , na hivyo masali yake yabaki yakiombewa
na kanda yote ya ziwa , kanisa lote la Tanzania na nchi za jirani, lakini pi aliwahasa
kuwa wasighafirike kwa kuwa hata mahali alipolazwa si mahali pake, mahali pake ni
pale alipomwandalia Kristo hili aweze kufurahi naye katika utukufu wake. Alimalizia
akisema Askofu Thadeus kwamba, Mungu amjalie utukufu pamoja na malaika na watakatifu
wote nasi atuombee.