Mkutano wa 13 wa Sinodi kwa ajili ya Uinjilishaji Mpya wawasilishwa rasmi kwa wanahabari
Asubuhi Ijumaa hii octoba 5, 2012, katika ukumbi wa Yohane Paulo 11, jengo la Uchapishaji
la Vatican, kuliwasilishwa rasmi kwa wanahabari , Mkutano wa XIII, Sinodi ya Kawaida
ya Maaskofu Katoliki. Sinodi hiyo itafanyika mjini Vatican tangu tarehe 7 hadi 28
Octoba 2012, chini ya Mada, Uinjilishaji Mpya: Uenezaji wa Imani ya Kikristu.
Uwasilishaji huo uliongozwa na Askofu Mkuu Nikola Eterovic, Katibu Mkuu wa Mkutano
huo.
Askofu Mkuu Etrovic akitoa muhtasari wa majadiliano ya Mkutano huo kwamba,ameeleza
kwamba, yote yamesimikwa katika maneno ya Yesu Kristu Mwenyewe,”Nendeni Duniani Kote
, Mkaitangaze Injili kwa kila Kiumbe” ( Mk 16,15).
Alisema. maneno hayo ya
Bwana Yesu Mfufuka, yaliyoandikwa mwishoni mwa Injili ya Mt. Marko, ni msingi wa
kazi na Utume wa Kanisa. Ni kwenda kuitangaza habari njema kwa watu wote. Ni agizo
la Yesu Kristu, linalo endelea kubaki daima lilelile jana, leo na milele, licha ya
mabadiliko ya nyakati au hali za kijami, kitamaduni, kisiasa, na kidini, kama tunavyoziishi
sasa.
Ni agizo la kitume kutoka kwa Bwana Mtufufuka, Mshindi wa dhambi na
mauti. Na ndilo litakuwa nguvu ya majadiliano yote ya Mkutano wa XIII wa Sinodi ya
Maaskofu. Kwa maneno hayo ya Yesu Kristu , na kwa kuzingatia waraka wa kufanyia kazi
uliopewa jina "Nyakati za Uinjilishaji Mpya", majadiliano yote yatalenga katika namna
ya kufanikisha agizo hilo la Yesu kufika katika kila kaya, kila utamaduni na mazingira.
AskofuMkuu Eterovic pia ameutaja mchakato huu kuwa mgumu na ni i shughuli
kubwa kwa Sekretarieti kuu ya Sinodi, hasa kuratibuna kuunganisha maoni na michango
ya washiriki. Kwa ujumla, katika mchakato huu una sura tatu zinazoingiliana, mtazamo
wa kiroho, kichungaji na kiteolojia.
Mama Kanisa ameweka tumaini katika sala
zilizoanzishwa tangu wakati wa maandalizi ya kazi hii, sala zilizoongezwa nguvu na
hija ya Baba Mtakatifu Benedikto XV1, katika madhabahu ya Loreto. Hija ya Alhamis
4 Octoba, ambako alikwenda kuomba msaada wa Mama Maria,ili wajumbe wwangaziwe na kutoa
maamuzi yatakayo wezesha kutoa matunda mazuri ya kuineneza Injili ya Kristu ambayo
ni Ujume wa upendo.
Na Jumapili 7 Octoba, Baba Mtakatifu Benedikto XV1,
ataongoza Ibada ya Misa ya Ekaristi kwa ajili ya ufunguzi wa kazi za Sinodi , ambamo
pia Papa atawataja watumishi wawiliwa Mungu, kuwa walimu wa Kanisa, Mtakatifu Giovanni
D’Avila na Idelgard di Bingen.