Vijana wasanii waalikwa kujiandikisha kwa ajili ya matamasha ya WYD 2013
Vijana kutoka pande zote za dunia , watakusanyika huo Rio de Janeiro kwa ajili ya
kushiriki kaitka adhmisho la Siku ya Vijana a dunia , itakayo fanyika Julai mwakani.
Vijana hayo si kwamba watakuwa mahujaji tu lakini pia iatkuw ni nafasi kwa
vijana kuifahamisha dunia juu ya uwezo wao katika sanaa, tamasha za kuigiza , michezo,
ngoma na muziki. Kwa ajili hiyo, hapo tarehe 15 Desemba 2012,wale wanaopenda kushirki
wanaweza kuanza kujiandikisha. Uadikishaji huo umetengwa katika makundi matatu ,
Muziki, wachoraji wa sanaa na tamasha. Masharti ya kujiunga katiak vikundi hivyo
yametolewa kwamba, wale wanao penda kushiriki katika tamasha la sanaa , utendaji
wa onyesho lao ni lazima uonyeshe sura ya mafundisho ya kanisa na ubora wa sanaa.
Na kwa wanamuziki , muziki huo ni lazima, uendane na mapokeo na mafundisho ya kanisa
Katoliki, ingawa kila kikundi kitatenda na kuimba kwa mahadhi ya utamaduni wao. Na
kwamba , baada ya makundi yote yanayotaka kushiriki kujiandisha, waandaaji wa WYD,
watachagua vikundi vitakavyoshiriki katika matukio hayo na vitatangazwa March 13
2013. Nwa kwamba, Sherehe hizi za sanaa , hazitaingiliana na Katekesi zitakazo
kuwa zikitolewa na matukio mengine yaliyoandaliwa rasmi kwa ajili ya WYD. Lengo la
maonyesho ya kisanii, ni kuanzisha mazungumzano kati ya imani na tamaduni, na asili
yake ni tangu mwaka 1997. Fomu za kujiandikisha zinapatikana katika tovuti ya
mtandao wa WYD 2013- Rio de Janeiro.