2012-10-04 07:46:14

Siku ya Pili ya kusikilizwa kwa Kesi ya kuvujisha nyaraka Vatican..


Kesi ya wizi wa nyaraka Vatican inaendelea kusikilizwa Vatican . Jumanne, ambayo ilikuw ani mara ya pili kusikilizwa kwa kesi hiyo inayomhusu Paulo Gabriel ,aliyekuwa msaidizi wa karibu wa Papa Benedikto XV1, anayetuhumiwa kuiba nyaraka binafsi za Papa , aliiambia mahakama kwamba, Pamoja na kutambua kwamba anamsaliti mwajiri wake, alilikuwa akivujisha vidogezo hivyo kwa mwanahabari mahalia, kama kujali kinachoendelea ndani ya Vatican. Na alifanya hivyo si kwa kushawishiwa na mtu mwingine ila maamuzi yake mwenyewe. Na akiulizwa kama aliwahi kumdokeza Papa yale yaliyokuwa yakimkera , alisema, hakuwahi kumwonyesha Papa vidokezo vya ndani alivyokwiba, wala kumdokeza Papa katiak mazunguzo.
Hata hivyo , alionyesha kujali kwake kwa watu kadhaa aliowaamini , kabla hajaanza kuiba vidokezo hivyo ,. Kati yao amemtaja Kardinali Angelo Comastri , Padre Mkuu wa Basilica la Mtakatifu Petro , Ingrid Stampa , Msaidizi wa Papa wa muda mrefu , Kardinali Paulo Sardi , aliyewahi kuwa Afisa katika ofisi ya Katibu Vatican na Askofu Francesco Cavina wa Carpi , pia aliyewahi kufanya kazi katika ofisi ya Katibu wa Vatican.
Kwa mujibu wa jeshi la Ulinzi wa Papa, Paulo Gabriel, kwa wakati huu, amewekwa peke yake katika chumba cha mahabusu cha Maaskari wa Vatican – “Gendarmeria Vaticana”. Chumba hicho cha mahabusu kiko katika hali ya kiwango kinachotakiwa kama ilivyo pia katika mataifa mengine ya Ulaya. Na anapata huduma zote , kuingana na viwngo vya mahabusu hiyo, kupata milo yote ya siku akiwa pamoja na maaskari wa zamu, wanao hudumia mahabusu, pia anapata wakati wa kupunga upepo na mapumziko na hata kuchanganyikana na maaskari walinzi wa Papa kwa barizi . Na kama anahitaji huduma za daktari pia atapata bila shida, na pia amepewa nafasi ya kupata huduma za kiroho. Ameshauriwa pia kupata vipindi virefu vya mapumziko , ili kuondoa hali za kumtia wasiwasi na hofu. Na pia anaweza kushiriki Ibada ya Misa akiwa na familia yake na pia ruhusu ya kukutana na Mkuu wa Ulinzi ,kufarijika. .










All the contents on this site are copyrighted ©.