2012-10-04 16:19:07

Madhabahu ya Loreto ni barabara ya wote- Papa


Baba Mtakatifu Benedikto XV1, akiongoza Ibada ya Misa katika uwanja wa Mama Maria wa Loreto, amesema, imani inapaswa kumfanya binadamu aishi kwa amani na utulivu , na kutembea katika njia ya sahihi ya maisha. Na kwamba Nyumba Takatifu ya Loreto, ni somo muhimu, na nuru inayoonyesha namna ya kutembea katika barabara hiyo.

Papa aliendelea kuitaja Nyumba hiyo Takatifu, kuwa ni kuwa ni ujumbe wa umoja. Amesisitiza , Hii si nyumba binafsi, wala si mali ya mtu au familia, lakini ni nyumba iliyo wazi kwa wote. Na hivyo inakuwa ni barabara kwa ajili yetu sote.

Papa aliendela a kuzungumzia Nyumba hiyo ambayo huwafanya watu watembee na kuishi ndani yake , kama lilivyofanya kundi la vijana 50 waliojiunga katika matembezi ya kuelekea Loreto toka pande mbalimbali za Italia, majimbo na parokia, akiwemo yeye mwenyewe Papa toka Vatican hadi Loreto, kwamba , inatukumbusha kwamba sisi wote ni wasafiri, tuko njiani kuelekea nyumba nyingine, katika mji wa hatima, mji wa milele, ambayo makao ya Mungu na binadamu waliokombolewa (taz. Ufu 21:03).

Papa aliendelea kueleza juu ya fumbo la Neno kumwilishwa, na kukaa kati ya binadamu, akisema, inashangaza daima. Mungu anatoa hoja yake na kusubiri binadamu afanye uchaguzi wake kwa hiari, Mungu anasubiri jibu kutoka kwa binadamu aliyemuumba yeye bure, anampa uhuru wa kuchagua, akiomba Mwana wake pekee amwilishwe ili aje kukaa kwetu na kutukomboa. Ni maajabu. Na Mama Maria anatoa jibu lake la ndiyo kwa kwa uhuru kamili .

Papa aliendelea kufanya nukuu kwa Mtakatifu Bernard wa Clairvaux, katika moja ya mahubiri yake maarufu yanayotumika sana, amabamo ameelezea, kukutana na Neno wa Mungu na Binadamu, akisema, inaonyesha " matarajio ya Mungu na binadamu katika jibu la "ndiyo" la Bikira Maria, aliyemgeukia Malaika kwa unyenyekevu , na kusema ndiyo , nitendewe kama ulivyonena, Na Malaika katika saburi,anarudi kwa aliyemtuma.

Kwa maelezo hayo, Papa ametoa mwaliko kwa watu wote, akisema kwamba, Mungu yupo anasubiri tutoe jibu, kama ilivyokuwa kwa Bikira Maria. Bila shaka, "ndiyo" ya Bikira ni matokeo ya neema ya kimungu. Hivyo tunajifunza Neema haiondoi uhuru, bali hujenga na kudumisha uhuru. Na Imani haimwondolei kitu binadamu lakini humwezesha kupata utambuzi kamili.

Papa alimalizia homilia yake na maelezo juu ya hija iliyofanywa na Mtagulizi wake Mwenye Heri Yohane XXIII, miaka 50 iliyopita akisema kwamba, ilikuwa ni kudra ya Mungu, kufanyika katika tarehe hii kukumbuka kwa Mtakatifu Francis wa Assisi, kwa hakika Injili ni hai.

Papa alitumia nafasi ya mahubiri pia kukabidhi kwa Mungu, hali zote ngumu za maisha katika dunia ya leo , inayotafuta kupata utulivu na amani , matatizo ya familia zilizo zongwa na hali za wasiwasi kwa ajili ya siku za baadaye , hamu za vijana wanaotafuta kujua maana ya maisha na wateswa wanaotafuta mahali pa kukimbilia na wale wanaochagua kuishi kwa mshikamano na upendo .

Pia Papa alikabidhi yote katika uaminifu wa Mama wa Mungu, yote yatakayofanyika kipindi hiki cha Neema za Kanisa ambazo zitajifunua hivi karibuni.

Papa amesali " Maria, Mama wa "ndiyo," uliyemsikiliza Yesu na kuzumguza nae tufundishe namna tunavyoweza kutembea katika njia ya imani na kumfuata Mwanao Yesu Kristu. Tusaidie Mama Kumtagaza ili kila mtu anaweza kukubali na kuwa mshiriki wa makao ya Mungu . Amina!








All the contents on this site are copyrighted ©.