Katika sala tunagundua utambulisho wetu wa kina kama Wakristu- Papa
Katekesi ya Papa ayendelea kuzungumzia sala ya Muumini. "Wapendwa ndugu zangu
wake kwa waume, leo ninapenda kueleza juu ya asili ya sala za kiliturujia kwamba,
liturujia ni kushiriki katika sala ya Kristu mwenyewe aliyoitolea kwa Baba ndani ya
Roho Mtakatifu, kama inavyofundisha Kateksimo ya Kanisa Katoliki , kipengere namna
1,073. Ni maneno yaliyofungua Katekesi ya Jumatano ya Baba Mtakatifu Benedikto XV1,
kwa Mahujaji na wageni, majira ya asubuhi mjini Vatican. Papa aliangalisha maelezo
yake , kwa Kanisa kama Fumbo la Mwili wa Kristu uliounganisha nalo, katika matoleo
ya sala kwa Baba. Na kwa kujitambulisha lenyewe kwa Kristu katika sala yake kwa Baba,
tunagundua utambulisho wetu wa kina kama Wakristu, na wana wa Baba Yetu aliye Mbinguni.
Liturujia hivyo, inakuwa ni kukutana na Kristu mzima, kwa maana kwamba Kristu
na Kanisa lake. Kwa maana hiyo, liturujia inapata maana ya kushirikishana sala ya
aliye Hai na ulimwengu wa jumuiya ya wanao mwamini Kristu. Papa aliongeza, Sala
ni kitendo cha kutambua uwepo wa Mungu, tunamtolea maneno ya kanisa lenyewe na kujifunza
kuzungumza kwake na kupitia kwake Kristu. Kanisa katika liturujia ni lenyewe kweli,
kwa kuwa ni mahali ambamo Mungu huja kwetu na kuingia katika maisha yetu. Papa
alieleza na kutoa mwaliko kwa waamini kukumbuka kwamba, kipindi cha Ibada za Kiliturujia
hufanyika kwa ajili ya Mungu na si kwa ajii yetu , ni kazi yake na ndiye asili yake.
Kwa upande wetu ,alimalizia Papa, wakati wa sala ya liturujia ni lazima kujifunua
wazi katika maongozi yake na mwili wake yaani Kanisa. Baada ya Katekesi hii,
Papa alisalimia katika lugha mbalimbali nakuwapa baraka zake.