Mahakama ya Kimataifa mjini The Hague, hivi karibuni ilitoa hukumu ya kifungo cha
miaka 14 jela kwa Bwana vita, Thomas Lubanga, wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Na nchini Sierra Leone, Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Sierra Leone, iliyosikiliza
kesi ya Rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor, alimhukumu miaka 50 jela. Katika
kesi zote mbili , sehemu kubwa ya maoni ya umma wa Afrika, yalioonyesha kutoridhika
na hukumu hizo.
Kwa Thomas Lubanga, Waafrika wengi wanaona adhabu aliyopewa
ni nyepesi kulinganisha na uzito wa makosa aliyotenda. Na kwa Charles Taylor, wengi
hawakukubaliana na uamuzi wake wa kukata rufaa dhidi ya hukumu. Kesi zote mbili zinaonyesha
, ni kiasi gani Afrika inajitahidi kuifanya dunia iieleweke katika masuala haya ya
haki. Na tukiongeza katika wazo la wale wanaoamini kwamba , haki haitaweza kutendeka
hadi hapo utendaji wa haki ufanyike dhidi ya uhalifu wa wote, na si kwa ajili
ya Afrika, hali itabaki katika mkanganyiko wa jumla.
Ni kweli kwamba leo dunia
iko katika mageuzi nyeti na wakati mwingine bila hoja kimantiki. Wahalifu wanaweza
kujulikana lakini wale wanaowatuma kufanya hivyo wanabaki kuwa watu huru, pamoja na
nia na mifumo iliyo nyuma na uhalifu msingi ya uhalifu huo kuwa mambo yasiyo gusika.
Mbali na hilo, haki inabaki kuwa mchakato mgumu. Haikomi kutokana na hukumu kutangazwa,
bali huendelea kutafuta haki kamili, licha ya kiwango fulani cha ukali, unaoweza
kufanyika wakati wa kesi kusikilizwa na usawa katika uchaguzi wa adhabu.
Papa
Benedict XVI , mara kwa mara amezungumzia suala hili katika mtazamo wa dhamiri
kwa kila mmoja wetu. Taratibu za sasa za utandawazi, zinalazimu kushirikishana majukumu.
Hali hiyo inahitaji viongozi kutuongoza kwa mujibu wa sheria, kutenda kwa namna za
kutopandikiza ukosefu wa haki. "Vile vile, katika muktadha usio kuwa na umuhimu au
sababu za maendeleo duni ya kitamaduni, tunapata shida za mifumo hiyo kujirudia
rudia. Papa Benedict XVI, ameandika katika waraka wake wa Upendo katika Ukweli “
Caritas in Veritate (No.22).
Katika matukio yote mawili ya Sinodi Maalu m za
Maaskofu kwa ajili ya Bara la Afrika, Sinodi ya 1994 na ile ya mwaka 2009, Maaskofu
wa Afrika walisisitiza masuala ya amani Haki, na maridhiano, na kama ilivyo aswa katika
Waraka wa Dhamana ya Afrika “ Africae munus”, Benedict XVI anakumbusha kwamba, mchakato
wa amani na maridhiano, una wawajibisha wahalifu na kafara na pia mamlaka husika.
anayetenda wakosaji na waathirika kama vile mamlaka. "Kama ni kuwa na ufanisi,
maridhiano hyana lazima yaambatane na utendaji wa kijasiri na uaminifu : kuwajibisha
wote wale waliohusika na migogoro hii, wale wanaojihusisha na mifumo hii ya uhalibifu
wa kial aina na nia zao . Waathirika wana haki katika kweli na haki. Ni muhimu kwa
sasa na ya baadaye ya kusafisha kumbukumbu, ili kujenga jamii bora ambapo majanga
kama hayo hayarudiwi tena "(Africae Munus, No 21).
Wito wa Kanisa inaonyesha
hatua ya kuanzia na kutoa mwelekeo wa kufuata: Haki ya watu, wakati inaonekana katika
mchoko iweze kuchota nguvu na msukumo katika haki ya Mungu, ambayo inatoa "upeo wa
macho ambayo ni lazima huwa kama ni kuwa mkamilifu, "(Africae Munus, No 25). Na kuwa
upeo kutoka kwa Mungu Mkamilifu, ambaye ni upendo, haki tu inayoweza kuongoza katika
misingi, isiyopandikiza hasira, kukanganyikiwa au chuki. Na iwezekane kwa viongozi
kueleweka , na Iwezekane kwa watu na hasa wabatizwa, kuishi katika maisha yao ya
kila siku.
Imeandikwa na Albert Mianzoukouta, Idhaa ya Kifaransa Afrika, Radio
Vatican.