2012-09-26 16:22:27

Jimbo la Papa, lasikitikia wingi wa vifo vinavyotokana na uzazi


Askofu Mkuu Silvano Tomas, Mwakilishi wa Kudumu wa Jimbo la Papa katika Ofisi za Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya Kimataifa ya mjini Geneva , Jumatatu akishiriki katika kikao cha Baraza la Haki za Binadamu, ambalo lilijadili kipengere 8, alirejea azimio la mwaka 1993 la Vienna na mpango wa utendaji ambamo mnatajwa kwamba, kipaumbele cha kwanza ni kupunguza idadi ya vifo vinavyosababishwa na uzazi kwa watoto na wamama.
Askofu Mkuu Tomasi alionyesha masikitiko ya Jimbo la Papa kwamba , bado kuna idadi kubwa ya watoto na wanawake wanaofariki kwa sababu hizi za uzazi , kama ilivyoelezwa katika Ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu, yaani, kwamba wanawake 287,000 walikufa kutokana na matatizo ya uzazi na kati ya 10 na milioni 15 ya wamama wengine walikabiliwa na mateso na udhoofu kutokana na uzazi katika kipindi cha 2010. RealAudioMP3









All the contents on this site are copyrighted ©.