Tanzia: Kardinali Fortunato Baldelli amefariki dunia.
Mama Kanisa anasikitika kutangaza kifo cha Muadhama Kardinali Fortunato Baldelli kilichotokea
hapa Roma, usiku wa kuamkia Ijumaa hii, 21 Septemba 2012. Marehemu Kardinali Baldelli,
ni mzaliwa wa Italia. Baba Mtakatifu Benedikto XV1, mara baada ya kupata taarifa
za msiba huu, alipeleka salam zake za rambi rambi kwa kwa njia ya telegram kwa familia
ya Marehemu kupitia kaka yake Mons. Piero Baldelli. Papa ameonyesha masikitiko
ya kuondokewa na mtumishi huyu wa Mungu , aliye mweleza maisha yake yalitoa ushuhuda
hai wa imani kwa Kristu, katika hali zote, maisha ya kawaida na maisha ya Kipadre.
Pia Papa ametaja juhudi na uaminifu wake kama mwakilishi wa jimbo la Papa, katika
ngazi ya kidiplomasia, akilishwa na uvuvio wa kichungaji na imani thabiti katika
Injili. Papa amekamilisha rambirambi na maombi kwa Mama Bikira Maria na kwa Mtakatifu
Francis wa Assisi, ili Bwana aweze kuipokea Roho ya Marehemu katika ufalme wake wa
uzima wa milele. Pia Papa ameomba baraka na faraja za Bwana, ziwashukie na kuwafariji
wote wanaoomboleza kwa uchungu msiba huu. Fortunato Baldelli, alipadrishwa March
18, 1961. Na aliingia katika huduma za Kidiplomasia za Jimbo la Papa mwaka 1966. Na
aliteuliwa kuwa Mjumbe maalum wa kudumu katika Ofisi za Jimbo la Papa za Baraza la
Ulaya kunako mwaka 1979. Na 12 February 1983, aliteuliwa na Papa Yohane Paulo 11,
kuwa Askofu Mkuu wa Jina wa Mevania, na kutumwa kama mjumbe wa Papa Angola. Na mwaka
1985 pia kutajwa kuwa mjumbe wa Papa Sao Tome na Principe. Cheo alichokitumikia
pia katika Jamhuri ya Domenican mwaka 1991 na Peru 1994 na baadaye Ufaransa kati ya
1999 hadi 2009, na hatimaye kuteuliwa kuwa Mkuu wa Baraza la Kitume la Kitubio , kazi
aliyoifanya hadi kustaafu Januari 5, 2012. Marehemu alikuwa bado ana haki ya kupiga
kura katika Conclave. Maziko Tamko toka Kanisa Kuu la Mtakatifu
Petro, linaonyesha Ibada ya Misa ya Marehemu kwa ajili yake, itafanyika Jumamosi
22 Septemba 2012, katika Altare ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro majira ya saa kumi
na mbili za jioni. Ibada hiyo, itaongozwa na Kardinali Angelo Sodano, Decano wa Dekania
ya Makadinali akisaidiana na Makardinali wengine na Maaskofu wakuu na Maaskofu.