2012-09-21 16:10:26

Papa akutana na Maaskofu wapya - Castel Gandolfo


Maaskofu wapya, wameaswa kujiepusha na tamaa za ujana,mabishano yasiyokuwa na msingi , bali wawe adilifu na imara katika imani na amani , wakishikamana na watu wote wanaomwomba Bwana kwa moyo safi( 2Tim-22-25.
Ni wito wa Baba Mtakatifu Benedikto XVI, wa siku ya Alhamsi kwa maaskofu wapya, alipokutana nao katika makazi yake ya Castel Gandolfo.
Hotuba ya Papa kwa Maaskofu wapya ilianza kuwaangalisha katika matukio ya hivi karibuni kwamba, kuzinduliwa kwa mwaka wa Imani, miaka 50 ya uwepo wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, miaka 20 ya Katekismo mpya ya Kanisa Katoliki na Mkutano wa 13 wa Sinodi ya Kawaida ya Maaskofu, ni matukio yanayopaswa kuhamasisha imani thabiti.
Aliwaambia Maaskofu, kwa ninyi kuwa Roma, kuanza utume wenu katika huduma ya kiaskofu, ni wakati muhimu wa kupata uzoefu thabiti katika haja ya kujenga umoja kati yenu ninyi kwa ninyi, na kukutana na Khalifa wa mtume Petro , kujilisha zaidi, maana ya uwajibikaji kwa ajili ya kanisa zima la ulimwengu.
Papa aliwaalika Maaskofu wapya kukuza na kuunga mkono kishawishi cha jumuiya ya Kanisa kupendelea kuwajibikaji zaidi na uinjilishaji mpya ili waamini waweze , kugundua furaha ya kumwamini Kristu, na kuiwasilisha imani hiyo kwa watu wengi zaidi .
Na kwamba wito huu ni kwa ajili ya kukuza na kulisha umoja na ushirikiano katika hali zote halisi za kijimbo . Uinjilishaji , aliendelea, si kazi ya watalaam, lakini ni kazi ya wana wote wa Mungu, wakiongozwa na wachungaji wao. Hivyo kila muumini anao wajibu katika umoja wa kanisa , kujisikia huru na wajibu, kutangaza na kushuhudia Injili ya Kristu.
Uinjilishaji mpya , ni tunda la Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican , na ndIvyo ilivyo kweli, Mwenye Heri Yohane XIII, wakati wa kukamilika kwa Mtaguso 11, alilitaja tukio hili kuwa ni Pentekste mpya itakayowezesha utajiri wa ndani wa kanisa kuchanua upya na kueneza utendaji wake wa kimama hata nje ya kanisa na shughuli zote za ubinadamu.
Hivyo wachungaji wa kanisa leo hii , Papa aliendelea, hurithi mafundisho haya katika utakatifu wake wa kiroho na mnamo chotwa toka ndani yake, majiundo ya wamini.
Papa amewahimiza Maaskofu wapya , kujenga tabia ya kuwajibika na utendaji wa lika mbalimbali za waamini na hali za maisha , kw akadri zinazvyo jiwasilisha, katika mitazamo muhimu ya kiimani, taratibu na mipango , inayolenga kutoa jibu pia katika hoja zinazojitokeza katika dunia yetu ya utandawazi na teknolojia.
Papa alimalizia kwa nukuu ya aya za Mtume Paulo kwa Timoteo 2,22-25, Jiepusheni na tamaa za ujana , fuata, uadilifu,imani, pamoja na watu wote wanaomwomba Bwana kwa moyo safi. Epuka ubishi wa kijinga na kipumbavu, kwa utambuzi kwamba hayo huleta ugomvi. ....








All the contents on this site are copyrighted ©.