Baba Mtakatifu Benedikto XV1, Jumanne alitaja majina ya wajumbe maalum 36 watakaoshiriki
katika Sinodi ya Maaskofu ya Kawaida , itakayofanyika hapa Vatican kwa muda wa wiki
tatu -7-28 Octoba 2012. Licha ya wajumbe walioteuliwa na Papa, pia kila Baraza la
Maaskofu Katoliki Kitaifa, litatuma mjumbe wake.
Sinodi hii itatafakari kwa
kina juu ya mada: Uinjilishaji Mpya, kwa ajili ya kueneza Imani ya Kikristu.
Toka Afrika wajumbe walioteuliwa na Papa siku ya Jumanne ni , Muadhama Kardinal
Polycarp Pengo wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam, Tanzania, mwingine ni Mhasamu Askofu
Mkuu John Onaiyekan wa Jimbo Kuu la Abuja, Nigeria na Askofu Menghsteab Tesfamariam
wa Jimbo la Asmara in Eritrea.
Papa Mwezi June, alitaja majina matatu ya
watakao kuwa Marais wa Sinod, nao ni Muadhama Kardinal John Tong Hon, wa Jimbo la
Hong Kong, pia Muadhama Kardinali Francisco Robles Ortega , wa Jimbo Kuu la Guadalajara
Mexico, Na Muadhama Kardinali Laurent Monswemgo Pasinya wa Jimbo Kuu la Kinshasa DRC.