2012-09-20 15:59:03

Ni dhambi kubwa kulazimisha muathirika kufunga kizazi


Viongozi wa kidini nchini Kenya wameonya kwamba, huduma za kulazimisha wanawake wanaoishi na virus vya HIV kufunga kizazi haZikubaliki , maana kufanya hivyo , ni kutenda kinyume na haki msingi za wanawake.
Viongozi wa kidini Kenya wametoa tamko hili kupitia mtandao kwa ajili ya watu wanaoishi na virus vya HIV na Ukimwi (KENERELA+). Viongozi hao wameonyesha kujali uwepo wa huduma hii, inayo fanywa kinyume na matakwa ya wanawake wanaoishi na virus vya HIV, walio bado katiak umri wa kupata watoto.
Viongozi wa Kidini wanasema huduma hiyo si tu iko kinyume na ubinadamu bali pia ni kuwanyanyapaa waathirika . Na hivyo wote wanaojihusisha na utoaji wa huduma hiyo mbovu, wawajibishwe kisheria.
CISA imetaarifu, Mstaafu Askofu Mkuu Benjamin Nzimbi wa Kanisa la Kianglikan Kenya , ameonyesha mshangao kwamba, huduma hii ya kufunga kizazi waathirika, inafanyika wakati huu ambamo sayansi imepiga hatua katika huduma za uzazi . Na hasa katika kuzingatia kwamba sasa wanawake waathirika wanaweza kujifungua watoto bila ya kuambukiza mtoto virus. Anasema, juhudi zozote za kumfuga kizazi mwanamke anayeishi na virus kupata mtoto ni uonevu na dhambi. .
Vivyo hivyo Askofu Patrick Mungai wa Kanisa la Kiinjili Kenya , pia amenukuliwa akilaani huduma ya kuwafunga kizazi waathirika wa virusi vya HIV, kwamba ni unyama na kinyume cha haki za biandamu, Hoja inayoungwa mkono pia na Sheikh Abdulllatif Abdulkarim Mratibu wa Maimamu wa Kenya na Ulamaa.
Viongozi wa kidini Kenya wametoa tamko lao kwa kurejea kifungu cha Kikatiba , kinachokataza mtu kulazimshwa kufungwa kizazi au kuhasiwa kwa nguvu. Kila Mkenya ni haki yake kikatiba kupata watoto kama wanavyopenda mwenyewe . Na kila Mkenya anayo haki ya kupata huduma bora za afya ikiwemo huduma za uzazi .








All the contents on this site are copyrighted ©.