Jumamosi iliyopita , mjini Nairobi, kulifanyika “Matembezi ya Harambee ya Kardinali
Otunga”,kama ilivyo andaliwa na Jimbo Kuu Katoliki la Nairobi Kenya , kwa lengo la
kuchagisha fedha kwa ajili ya ufanikishaji mchakato wa kumtaja Mtumishi wa Mungu Maurice
Michael Kardinali Otunga , katika daraja la Wenye Heri. Kati ya wafadhili wa matembezi
hayo , ilikuwa ni Benk ya Biashara Kenya(KCB). Matembezi haya yaliongozwa na
Muadhama Kardinali John Njue wa Jimbo Kuu la Nairobi. Wakati huo wa Matembezi, Muadhama
Kardinali John Njue aliwaomba waamini na watu wote wenye mapenzi mema, wajitoe kwa
ukarimu zaidi, kufanikisha juhudi hizi, kwa kuwa huhitaji fedha nyingi. Na KBC, ilitoa
hundi ya shillingi za Kenya , laki moja kwa ajili ya mfuko huu wa Kardinali Otunga.
Na Makamu Msimamizi wa mchakato huo, Bruda Reginald Cruz , akirejea matembezi
ya Jumamosi, aliiambia CISA kwamba, watu wengi waliweza kujitokeza kushiriki harambee
hii. Na kwamba fedha inayotafutwa ni kwa ajili ya kufanikisha awamu ya kwanza ya
mchakato huu, ambayo ni ngazi ya kijimbo. Na tayari wamekwisha fanya shughuli zingine
kwa lengo hilo, mfano uwepo wa mashindano ya mpira wa magongo na pia wamekwisha andaa
mlo wa jioni . Matembezi haya yalifungwa wka sala iliyoongozwa na Askofu Mkuu
Mstaafu John Jenga wa Jimbo Kuu la la Mombasa, ambaye pia aliwashukuru wote walioshiriki
matembezi haya.