2012-09-19 16:21:17

Papa atafakari ziara yake nchini Lebanon


Baba Mtakatifu Benedikto XV1, akikutana na Mahujaji na Wageni, mjini Vatican,kwa nia za kutoa katekesi kama ilivyo kawaida kwa Jumatano, hotuba yake ililenga katika ziara yake ya Kimataifa ya 24 ya hivi karibuni, nchini Lebanon. Papa alifanya ziara hii yakitume tangu Ijumaa 14 -16 Septemba 2012. Ziara inayotajwa kuacha alama kubwa ya utendaji wa jumuiya dogo ya Kikristu katika jumuiya kubwa ya Waislamu, Mashariki ya Kati.
Jumatano hii, Papa amerudia kutaja madhumuni ya ziara hiyo kwamba ,alikwenda kutia sahihi na kukabidhi waraka wake wa kitume, alioutoa kama matokeo ya Sinodi ya Maaskofu, aliyoiitisha maalum Desemba 2010, kwa ajili ya Kanisa Mashariki ya Kati. Na pia alikwenda Lebanon kwa nia ya kupeleka ujumbe wa amani, kwa watu wa Mashariki ya Kati , kupitia mikutano na wawakilishi wa makanisa mengine na jumuiya za kikanisa za Mkoa huo na pia viongozi wa dini ya Kiislamu.
Papa aliendelea kuonyesha furaha toka ndani ya moyo wake kwamba, alifanikiwa kusimama mbele ya watu wateswa wa matukio ya kusikitisha yanayolemea mkoa wa Mashariki ya kati, na kuhimiza utendaji wenye uvuvio wa amani katika eneo hilo.
Pia Papa amezungumzia kuguswa kwake na imani ya kanisa mahalia, ambako aliweza kutoa ombi kwa wawaamini kuendelea kukaza nyuso zao kwa Kristu msulubiwa, mwenye kuwa na uweza wote wa kuwapta nguvu na ushupavu wa kusonga mbele wakiwa wamejawa na matumaini thabiti katika Kristu , licha ya hali ngumu za majaribu yanayotaka kudhoofisha juhudi zao za kusherehekea ushindi wa upendo dhidi ya chuki , ushindi wa msamaha dhidi ya kisasi na ushindi wa umoja dhidi ya migawnyiko.
Aidha Papa kwa mara ingine alionyesha shukurani zake za dhati kwa jumuiya ya Kiislamu, na hasa kwa makaribisho mazuri na ukarimu mkuu kutoka kwa viongozi wa Kiislamu, wakimezesha kutoa pendekezo lenye ujumbe wa ujenzi wa majadiliano na ushirikiano miongoni wa jamii yote ya Lebanon na Mashariki ya Kati kwa ujumla.
Mwisho, Papa hakucehelea kuwashukuru wote walishiriki katika kazi hii ya kufanikisha ziara yake Lebanon. Na kwmba anaendelea kutoela sala zake kwa mkoa huu mpendwa wa Mashariki ya Kati. Na aliomba msaada wa Mama Bikira Maria , kufikisha maombi ya watu wa eneo hili, lenye kuwa na madhabahu nyingi za kale, ili haki na amani vipatikane kwa ajili ya watu wote wa Mashariki ya Kati.








All the contents on this site are copyrighted ©.