Pamoja na uwepo wa changamoto ngumu, Kanisa bado lina matumaini makubwa katika vyama
vya kitume na jumuiya mpya za Wakristu, ambamo mhemko wa imani hulishwa na karama
za waumini wenyewe. Katika kuadhimisha mwaka wa Imani , si kama ni tukio la kushereheka,
bali ni mwaka wa neema ya Bwana , zawadi inayopaswa kupokelewa kwa moyo wa shukurani
na uchaji na uwajibikaji kwa watu wote. Ni tafakari ya Muadhama Kardinali Stanslaw
Rylko, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Walei, kwa wakati huu, tunapo elekea
kuuanza mwaka wa Imani , utakaoanza Octoba mwaka 2012. Ameuita ni Kipindi cha kuzama
katika “ Safari ya Imani” na kuruhusu kugundua upya kila siku, uzuri wa safari hii
ya imani, inayoelekeza katika kumgundua Mungu wa Kweli. Anasema, " Harakati za
kikanisa na jumuiya mpya - pamoja vyama vingine ya walei katika Kanisa leo hii, kweli
ni "maabara ya imani"au "shule za imani"kwa kuwa ni , mahali ambamo vijana, watu wazima,
wenye ndoa , huweza kutembea pamoja katika njia ya kukutana na Mungu kupitia Yesu
Kristu. Na kama anavyoeleza Zygmunt Bauman kwamba , jamii ya leo, ni jamii iliyomezwa
na utamaduni wa maonevu, na kuifanya dunia kuwa mahali pasipokuwa na uhakika wa maisha,
maisha yasiyokuwa na kumbukumbu wala rejea, isipokuwa kumezwa harara za mambo ya
mpito kama fedha, anasa na mali, maisha ya kukanganyikiwa. Kardianli Rylko anaasa,
kwenye hali hizo, harakati za kikanisa na jumuiya mpya kuiimarisha imani yake kwa
Kristu , linakuwa ni jambo lisiloweze kukwepeka, kwa ajili ya ujenzi wa ukomavu thabiti
katika imani. Na hivyo , bila shaka, nafasi hii ya mwaka wa imani , itakuwa ni wakati
wa kila mumini kupima imani yake na kuiimarisha zaidi ili aweze kupambana na changamoto
zinazomkabili kama yeye mwenyewe binanafsi na kanisa kwa ujumla. Hata hivyo Kardinali
Stanslaw Rylko anasema, utendaji huu thabiti katika imani ni sehemu ya uhuru kila
binadamu, unaomhitaji kukaa macho na mambo yanayoweza kuvuruga imani yake. Hivyo basi
Mwaka wa Imani, si kama kipindi cha kushereheka, bali ni mwaka wa neema ya Bwana
, zawadi nyeti toka kwa Mungu , inayopaswa kupokelewa kwa moyo wa shukurani, uchachi
na hisi za uwajibikaji kwa waamini wote.