Uwepo wa Kanisa iwe ni Ishara ya Amani - asema Papa katika Mkutano wa Kiekumene :
Jumapili majira ya saa kumi za joni, Papa aliuhutubia mkutano wa kiekumene, katika
monesteri ya Mama Yetu wa ukombozi ya Charfet, ya Upatriaki Katoliki wa Siro. Mkutano
uliohudhuriwa na wawakilishi wa makanisa mbalimbali, na likiwa tukio la mwisho muhimu
katika ratiba ya ziara ya Papa Lebanon. Mkutano ulio andaliwa na Patriaki Youssuf
Younan, wa Kanisa Katoliki la Siro, katika mtazamo kwamba, ziara hii ya Papa, na
iwe chimbuko la kazi za kuleta umoja kamili kwa wafuasi wa Kristu. Papa akihutubia
mkutano huo, Papa alikiri kuona ushuhuda wa imani, unaoendelea kuonekana katika Kanisa
Siria ya Antiokia, kama ilivyo katika historia yake tukufu ndefu, yenye kushuhudia
upendo motomoto kwa Kristu, ushuhuda ulioleta mhemko wa kuandika nyaraka nyingi za
kihistoria, juu ya utendaji wa kishupavu, hata kuyatolea maisha mhanga , wakibaki
na imani thabiti mioyoni mwao.
Papa alieleza na kuhimiza kwamba, uwepo wa
kanisa uwe kwa ajili ya watu wa mkoa huu kama alama ya amani inayotoka kwa Mungu na
pia kama mwanga unaowadumisha katika tumaini hai.
Na kwamba kukutana kwake
wajumbe hao, ilikuwa ni ishara inayo onyesha nia thabiti zinazolenga kutoa jibu
kwa ombi la Kristu “kwamba wote wawe na Umoja” (Yn 17:21). Papa aliendelea kutaja
hali halisi za nyakati hizi ambamo vurugu na ghasia zimepamba moto , akisema, inakuwa
ni jambo la muhimu, kwa wafuasi wa Kristu, kutoa shuhuda thabiti katika umoja wao,
ili dunia iweze kuusadiki ujumbe wa Kristu, kwamba ni maisha ya upendo , amani na
mapatana maridhiano. Wakristu wanapaswa kuona kwamba, katika kuikiri imani na kubatizwa,
walichukua dhamana ya kuufika ujumbe huu wa thamani kubwa katika maisha ya watu dunaini
kote hasa Mashariki ya Kati.
Papa amewasihi Wakristu wasichoke kuuishi upendo
huu wa Kristu , ili hatua kwa hatua waweze kufika katika umoja kamili. Kwa ajili hiyo,
Papa alihimiza sala za pamoja na uwajibikaji wa pamoja, na kwa maombezi Mama Bikira
Maria kwa Mwanae, waweze kufanikisha nia ili kila binadamu aweze kukombolewa dhidi
ya uovu na ghasia, na hivyo Mashariki ya Kati yote maisha ya watu yarudie maridhiano
na amani.
Papa alihitimisha na maneno : Nawaachie amani , nawapeni amani yangu(.
Yn 14, 27), na yawe maneno na ishara ya kila mmoja inayotolewa katika jina Kristu
kwa watu wa mkoa huu mpendwa, katika hamu ya kuona maneno hayo yametimia! Asante!