Jumapili Papa alikamilisha ziara yake ya Kitume ya 24 Kimataifa Lebanon
Baba Mtakatifu Jumapili alikamilisha ziara yake ya siku tatu nchini Lebanon(14-16
Septemba 2012), kwa maneno ya shukurani kwa wenyeji wake na huku akionyesha matumaini
ya kurudi tena Mashariki ya kati.
Katika muda huu wa siku tatu , ijumaa hadi
Jumapili, alikutana na watu na makundi mbalimbali, viongozi wa kidini na kisiasa
na pia lika la vijana, kwao wote akifikisha ujumbe wa amani na mapatano, kama yalivyo
mapenzi ya Bwana wetu Yesu Kristu. Nia nyingine kuu ya ziara hii ilikuwa kukabidhi
waraka wake wa kitume , ambao ni matokeo ya sinodi ya Maaskofu maalum, aliyoiitisha
Desemba 2010, kujadili hali ya maisha ya Kanisa Mashariki ya Kati.
Papa kabla
ya kuianza ziara hii, baadhi ya watazamaji wa mambo walionyesha kuhofia usalama wa
Papa kutembelea Mashariki ya Kati , kipindi hiki ambamo kuna mnajitokeza matukio
ya ghasia za waislamu wenye siasa kali, kushambulia Wakristu, na migogoro ya kisiasa
yeney kusabab isha uwamgajiwa damu .
Papa akizungumza na wanahabari wakati
akeilekea Lebanon aliwaambia , pamoja na hali za machafuko na ghasia zinazofanywa
kwa wakati huu , hakuwa na wazo la kuifuta ziara hiyo. Alisema, wakati wa hali hizi
za wasiwasi mwingi na mashaka,ndiyo unakuwa wakati muafaka wa kukutana na kujadiliana
, mbinu za kuondoa hali hizo.
Na wakati akiangana na wenyeji wake katika
uwanja wa ndege wa Beirut, Papa alionyesha matumaini yake kwamba, ziara yake imeweza
kuionyesha dunia kwamba, inawezekana Wakristu na Waislamu kuishi pamojakwa amani na
mshikamano. Na alitoa shukurani zake za dhati kwa Waislamu wote waliofika kumlaki
na kumsikiliza, na kufanikisha safari yake.
Na alirudia kukazia wajibu wa
Lebanon kwa Mashariki ya Kati, ni kuzidi kushuhudia kwamba, inawezekana wafuasi wa
dini , imani na tamaduni mbalimbali kuishi pamoja kwa amani na utulivu. Papa alieleza,
akiitaja Lebanon, tangu kale imo katika eneo la madhabahu Matakatifu ya Mungu. Na
aliomba Lebanon na watu wake hata leo hii, waendelee, kuishi kwa amani na utulivu
, ndani ya eneo hili linalotambulika Kama madhabahu Matakatifu ya Mungu. Papa awasalimia
Wakarmalite kabla ya kuelekea Uwanja wa Ndege.
Jumapili , Baba Mtakatifu akielekea
Uwanja wa ndege, alisimama kwa muda wa dakika kumi hivi katiak monestri ya Wakarmalite
wa Mama wa Mungu, kuwajulia hali na kuwatia shime katika utume wao wa kuwa alama y
aumoja na mshikamno nchini Lebabon.
Papa alipokelewa na Mama Mkuu , Tereza
wa Mtoto Yesu , mhispania ,ambaye ni kati ya waanzilishi wa nyumba hiyo,waliyoianzishwa
miaka 50 iliyopita. Papa alitolea sala katiak jengo dogo la kanisa mahali hapo nakusikiliza
wimbo mfupi wa Masista hao. Na aliwabariki na kwuapa zawadi ya Mama Maria akiwa na
Mtoto Yesu. Na mwisho alibariki jiwe jipya la msingi litakalowekwa katiak jengo jipya
la shirika hilo, linalotazamiwa kujengwa huko Cana Lebanon.