Siku ya kwanza ya ziara ya Papa yafanikiwa - Pd. Lombardi
Mapema Jumamosi, Padre Federico Lombardi, msemaji wa Vatican, akitoa muhtasari wa
siku ya kwanza ya ziara ya Papa ameeleza kuwa , siku hiyo ilijaa mikutano mingi na
yote ilikwenda vyema. Papa aliweza kutoa jibu la swali la kwanza muhimu katika ziara
hii. Jibu lililoweza kutoa wasiwasi na mashaka mengi yaliyokuwepo , kulingana na hali
halisi za machafuko yanayojitokeza hapa na pale , ikiwemo mivutano ya kidini katika
Mkoa wa Mashariki ya Kati . Mara kwa mara Papa alirudia kutaja , nia na lengo
la ziara yake kwamba ni kupeleka ujumbe amani na kuimarishana katika ujenzi wa
amani. Na kwamba , hotuba ya Papa Uwanja wa Ndege, ililitaja taifa la Lebanon,
kuwa mfano kwa mataifa, yenye kuwa na tamaduni na dini mbalimbali, kuweza kuishi
pamoja , katika hali ya mshikamano na maelewano . Na kwa upande wa utume wa Kanisa
katika jamii, Papa amesisitiza zaidi wajibu wa walei katika kuwa mashahidi wa amani
. Na amehimiza Wakristu kuziishi sheria za nchi na kushiriki shughuli za kitaifa kama
ilivyotamkwa katika katiba ya nchi, na kulingana na mafundisho ya Kanisa ya kijamii.
Aidha ametoa wito, kuvishinda vishawishi vyenye kuelekeza katika migawanyiko
ya kijamii. Badala yake jamii ijali zaidi kutafauta majawabu kwa njia za mazungumzano
na maelewano iwapo panajitokeza hali za kutofautiana kifikra. Na kwamba Ukristu si
dhana ya mabavu, bali ni njia ya majadiliano katika ujenzi wa jamii yenye maelewano
na mapatano.