2012-09-15 13:43:42

Papa akutana na Viongozi wa kiserikali , wabunge na wanadiplomasia


Jumamosi, 15 Septemba 2012, kabla ya adhuhuri, Baba Mtakatifu amekutana viongozi wa kiserikali , akiwemo Rais Michel Sleiman, wa Lebanon , wawakilishi kutoka Bunge na mamlaka za kitawala Lebanon Wakuu wa tume za Kidiplomasia, akiwepo pia Mwenye Heri Partiaki Béchara Boutros Rai, na viongozi wengine wa Kidini , Maaskofu na watu wengine mashuhuri wake kwa waume. Mkutano huu ulifanyika katika jengo la Ikulu la Baabda.
Kabla ya kuingia katika mkutano huu, Papa alipanda mti mdogo wa Mkangazi, aliouita alama ya uzuri wa taifa la Lebanon. Na maelezo yake mafupi katika tukio hili , alisema, huduma nzuri inayohitajika kuukuza mti huo hadi kupanuka na kuwa na matawi mengi , iwe ni ishara ya hitaji la huduma nzuri kwa wakazi wote wa Lebanon na Mkoa wote wa Mashariki ya Kati , kwa sasa na tumaini lao la baadaye. Na kwamba anaendelea kumwomba Mwenyezi Mungu aibariki Lebanon na watu wakazi wote wa eneo hili, lililoshuhudia kuzaliwa kwa dini kuu na tamaduni zao . Papa alihoji kwa nini Mungu alilichagua eneo hili la Mashariki ya Kati ? Na kwa nini sasa watu wake wanateswa na machafuko?
Papa ametoa jibu, akionyesha imani yake kwamba, Mungu alilichagua eneo hili , ili liweze kuwa mfano, na shahidi mbele za dunia, kushuhudia kwamba, kila binadamu , mke au mme anao uwezo wa kupenda amani na mapatano, kama sehemu ya uvuvio wa mpango wa Mungu, uliozamishwa katika roho ya kila binadamu, aliyeumbwa kwa sura na mfano wake Mungu.
Katika mkutano huu , Papa ametaja hamu yake ya kupenda kuzungumzia amani , iliyoletwa na Yesu Kristu.
Na alianza kwa kuonyesha shukurani zake za dhati kwa Rais Michel na kwa wote , kwa mwaliko na makaribisho mazuri yake. Na alikumbusha kwamba, sifa na utajiri wa taifa lolote, hutegemea wakazi wake. Vivyo hivyo ndivyo ilivyo , hata mustakabhali wa taifa umo mikononi mwa watu iwe mtu mmoja mmoja au kwa ujumla hasa katika utendaji wao, katika ujenzi na udumishaji wa amani. Na uwajibkaji katika amani unawezekana tu iwapo jamii,i itaishi kwa mshikamano na umoja.
Mshikamo wa kijamii unahitaji kukumbatia tunu zote zilizomo katika kutambua na kuheshimu utu wa kila binadamu na kuwajibika kushiriki katika utoaji wa mchango unaohitajika kwa akili na uwezo wote wa mtu. Na nguvu zote zinazohitajika kujenga na kuimarisha amani, pia daima hudai kufanya rejea katika chimbuko la ubinadamu.
Katika ukweli wake, ubinadamu wa mtu hautengani na maisha matakatifu, ambayo ni zawadi takatifu kutoka kwa Muumbaji. Katika mpango wa Mungu, kila binadamu ni peke na hana mbadala. Binadamu anayezaliwa ndani ya familia , ambayo ni shule ya kwanza ya ubinadamu na hasa ni shule ya kwanza katika ujenzi wa amani. Hivyo kwa ajili ya kujenga amani, Papa alisisitiza, tunahitaji kuitazama familia, kuisaidia na kuitetea na kuiwezesha katika utendaji wake.
Kwa namna hiyo utamaduni wa maisha hudumishwa . Na pia uwajibikaji wa binadamu katika amani hutegemea juhudi za binadamu kuelewa maana ya kina ya maaisha. Kama tunapenda amani ni lazima kutetea maisha. Mtazamo huo, huongoza katika kukataa si tu vita , ghasia na ughaidi lakini kila aina ya madhulumu yanayoweza kufanywa ddhdi ya maisha yasiyokuwa na hatia ya binadamu, wake kwa waume, kama viumbe wa Mungu.
Papa ameasa, kila mara, pale ukweli wa asili ya binadamu unapopuuzwa au kukataliwa , hapo ndipo inapokuwa vigumu kuheshimu asili hii,iliyoandikwa katika moyo wa kila binadamu.
Papa aliendelea kuitazama hali ya baadaye ya vizazi vijavyo , akitoa mwaliko kwa wote kwamba , ni wajibu wa kizazi cha sasa kuelimisha juu ya amani, kwa ajili ya ujenzi wa utamaduni wa amani. Elimu hii , iwe majumbani au mashuleni ni lazima iwe imesimikwa katika misingi ya tunu za kiroho ambamo mna hekima na busara zote za kila utamaduni na maana ya maisha.








All the contents on this site are copyrighted ©.