Uhuru wa kidini Kimataifa ni sharti msingi kwa ajili ya amani na manufaa ya wote.
Hakikisho la uhuru wa kidini ni dhamana ya maisha adilifu yenye utulivu na amani miongoni
mwa jamii . Ni Mchango wa Askofu Mkuu Silvano M. Tomasi, Mtazamaji wa kudumu wa jimbo
la Papa katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Geneva , alioutoa siku ya Jumatano, wakati
akichangia katika mkutano wa Kimataifa juu ya Uhuru wa Kidini, uliofanyika huko Washington
Marekani, kuzungumzia hali halisi za uhuru wa kidini katika nyakati hizi. Amesema
uhuru wa kidini sasa ni dharura muhimu leo hii, kama inavyojionyesha wazi pia kwamba,
uhuru wa kidini imekuwa ni kati ya hoja zinazo jadiliwa mara kwa mara katika mikutano
na midahalo. AskofuMku Tomasi aliendelea kusema, na ndivyo ilivyo ukweli kwamba,
Uhuru wa Kidini, uko katika hali za kugandamizwa duniani. Alieleza kwa kurejea takwimu
zinazoonyesha kwamba, asilimia 70% ya watu duniani, wanaishi chini ya mashinikizo
ya masharti ya kidini. Zaidi wa watu billioni mbili, ikiwa karibia moja ya tatu ya
idadi ya watu duniani , wanaishi katika hali ambazo madhulumu yanazidi kuongezeka,
hasa katika miaka ya hivi karibuni, yakionekana mashambulio waziwazi kimwili , uharibifu
wa mali na vitu vya kidini. Pia amekumbusha ni wajibu wa watu wote kuzingatia
uhuru wa kidini , kama lengo la kwanza katika utendaji wote wa kila siku. Kwa Wakristu
hakuna mjadala katika hilo. Maelezo ya AskofuMkuu Silvano Tomasi aliyaangalisha
katika matukio mbalimbali ya kusikitisha katika madhulumu haya kidini, yaliyofanyika
hivi karibuni katika mataifa mabalimbali, Nigeria, Kenya Iraki, Siria n.k. yakimfanya
mtu atafakari kwa kina suala hili la uhuru wa kidini , na waamini kuheshimiana mmoja
kwa mwingine. Na kwamba inavyoonekana mara nyingi madhulumu yamekuwa mabaya zaidi
katika mataifa ambako kuna sheria zinazo tetea uhuru wa kidini na hasa sheria inayokataza
kashfa dhidi ya mambo ya kidini, sheria hiyo inaonekana kutumika kama kinga ya kudhulumu
makundi madogomadogo ya kidini, mfano uwepo wa jumuiya ndogo ya Wakristu katika mataifa
yenye kuwa na Waislamu wengi, au pia kundi dogo la Waislamu katika jumuiya nyingine
kubwa. Hotuba ya Mosinyori Tomasi , inaendelea kuangalisha katika hali mbalimbali
za mataifa hata uhuru wa kidemokrasia katika mataifa ya Magharibi ambako dini inapenda
kuchukuliwa kama ni suala la mtu binafsi, ikisahauliwa kwamba, dini ni chimbuko la
uhuru wa kweli wa mtu. Kwa mtazamo huo, kuna mwelekeo wa agenda za kisiasa matokeo
yake ni kuwa na uhuru usiokuwa na mipaka na siasa zilizo kinyume na dini. Sheria zisizojali
misingi na sheria za maadili katika asili ya binadamu mfano familia na maisha manyoofu
matakatifu. Pia kutakana na uhuru huu usiokuwa na mipaka wala uadilifu, vinaendelea
hata leo hii, kuendeleza enzi ya watu kufia dini hata katika nyakati zetu. Kardinali
amekumbusha kwamba Mwezi March , Baraza la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya haki za binadamu
, lilirudia kwa mara nyingine kutaja azimio linalotetea utetezi wa uhuru wa kidini,
kama ilivyokwisha tamkwa tena kwa mara nyingine mwaka 1981 na mwaka 1986, kama kutoa
msisitizo wa nguvu katika kuhakikishauhuru wa kidini unaheshimiwa katika ngazi zote
tangu kwa mtu binafsi, watu wote kwa ujumla na katika ngazi za kitaasisi na kimataifa.hakikisho
la uhuru wa kidini hutoa mchango wake katika dhamana ya kuheshimu tunu za uadilifu,
msingi wa uhuru wa kidini kwa kila biandamu. Amesisitiza Askofu Mkuu Silivano Tomasi