Baba Mtakatifu Benedikto XV1, mapema Ijumaa hii anaianza safari ya kitume ya 24 Kimataifa
kuelekea Lebanon, safari inayolenga kumkutanisha na Kanisa Mashariki ya Kati , ambako
pia atatoa waraka wa mwisho wa Sinodi ya Maaskofu ,iliyofanyika Maalum kwa ajili ya
Mashariki ya Kati. Hii ni ziara ya siku tatu 14-16 Septemba 2012. Papa Benedikto
XV1,anakuwa ni Papa wa tatu kutembelea Lebanon, akiwa ametanguliwa na Papa Paulo V1
, aliyezuru Lebanon tarehe 2 Desemba 1964 . Na Papa Yohane Paulo 11 aliyetembelea
Lebanon tarehe 10-11 May 1997, ambako aliwasilisha hati ya mwisho juu ya Sinodi ya
Maaskofu, iliyozungmzia Tumaini Jipya kwa Lebanon. Ziara ya Papa Benedikto XV1,
Lebanon imejengwa katika matumaini ya kuimarisha Kanisa Mashariki ya Kati na kutoa
tumaini jipya kwa vijana , na mwamko mpya katika mazungumzano ya kiekumene, na kati
ya Waislamu na Wakristu, katika lengo la kuwa na maisha ya amani maelewano na tulivu
. Lebanon, ambayo ina jumuiya ya Wakatoliki ni kubwa, ilichanguliwa tangu mapema,
hata kabla Syria haijaingia katika machafuko ya kisiasa, yenye umwagaji wa damu yanayoendelea
sasa. Papa baada ya kukamilisha waraka wa mwisho juu ya Sinodi ya Maaskofu Maalum
kwa ajili ya Kanisa la Mashariki, sasa anakwenda kuuwasilisha, , kama matokeo ya sinodi
hiyo na utatumika kama mwongozo wa utendaji wa Kanisa Katoliki Mashariki ya Kati.
Waraka ambao ni majumuisho ya maoni ya wajumbe waliokutana katika sinodi hii ambayo
ilikutanisha wajumbe kutoka jumuiya mbalimbali , si za Kikristu tu lakini pia Waislamu
na Wayahudi , kuzitazama hali halisi za maisha ya watu Mashariki ya Kati na hasa wahamiaji
na jumuiya ndogondogo za kidini na mtazamo mpana wa kuwa na uhuru kamili na demokrasia.
Sinodi hii ilifanyika kabla ya kile kinachoitwa mfumko wa ”Wimbi la Mapambazuko Uarabuni”.
Padre Federico Lombardi hivi karibuni katika tahariri yake ya wiki alisema,
kutokana na mabadiliko haya mapya, katika uwanja wa kisiasa katika Mataifa mengi ya
Mashariki ya Kati, ni wazi kwa sasa, kumejitokeza hoja ya kidharura katika utume wa
Kanisa katika eneo hilo. Hata kama hali ya uinjilishaji inaonekana bado kuwa ngumu
zaidi , hivyo, uwepo wa Papa katika eneo hilo, unatumainiwa kuwa msaada mkubwa katika
kuvuvia moyo wa mshikamano,amani na utulivu miongoni mwa jamii ya watu wa Mashariki
ya kati. Inaaminika Wakatoliki na Wakristu kwa ujumla , pamoja na uchache wao
katika mkoa huo, wanaweza kutoa mchango mkubwa kupitia shuhuda za maisha ya amani
na utulivu na ukuzaji wa majadiliano kupitia hali ngumu za mateso wanayoyaishi, na
si tu kwa vikundi vya dini zingine vinavyo zidi kuongezeka Mashariki ya kati , lakini
pia jumuiya ya kimataifa , kuona umuhimu wa kutoa jibu thabiti katika mivutano ya
dunia ya kisiasa, kijiografia au kimikoa. Papa anakwenda Lebanon , kutoa sauti
yake ya matumaini na hamu ya kuwa na amani katika mkoa wa Mashariki ya Kati. Kanisa
linatumaini kilio cha Papa kitasikilizwana watu w Mashariki ya katin a jumuiya ya
kimataifa kwa ujumla. Wakati wa ziara hii ya Papa Lebanon, Jumuiya ya Pax Christ,
ina waaalika watu wote, wakati wa siku hizi Papa kutembelea Lebanon, kufanya mafungo
na sala kwa nia ya kuombea amani Syria