2012-09-12 14:12:48

Watano wabaka na kuua mtoto wa kike- Pakistani


Madhulumu dhidi ya Wakristu yanaendelea kusikika Pakistan, licha ya viongozi mbalimbali wa kimataifa kukemea dhuluma hizo.
Fides imeripiti kwamba, Augosti 14, binti wa miaka 15 , alibakwa na kundi la wanaume watano na kuuawa kikatili karibu na mji wa Sahiwal Punjab. Ni tukio jingine lililoumiza roho za Wakristu, ambalo taarifa zake zililifikia shirika la habari la Fides , wakati Mahakama ikisikiliza kesi nyingine ya madhulumu ambamo mtoto Mkristu wa miaka 11 , mwenye udumuavu wa akili , kukamatwa na ameikashfu korani .
Habari inasema, kijana huyo Rimsha Masih , ambaye huwa na tabia cha kuchakura mapipani kutokana akili yake duni inavyomtuma, aliokota karatasi hizo za koran pipani.
Watetezi wake wanasema, ni ukosefu wa ubiandamu kumweka jela Rimsha, ambaye hata hajui kusoma wala kuandika. Hivyo karatasi hizo za koran alizokutwa nazo, kwake yeye Rimsha zinaokena hazina tofauti na vitu vingine alivyookota mapipani.
Kesi hii imevutia wengi , kutaka kujua hatima ya kijana huyo.








All the contents on this site are copyrighted ©.