2012-09-12 14:05:01

Ujumbe wa Papa kwa Kongamano la Kimataifa la Wakatoliki Walei-


Baba Mtakatifu Benedikto XV1, amepeleka saalaam na ujumbe wa matashi mema kwa washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Wakatoliki Walei Afrika, kupitia kwa Kardinali Stanslaw Rylko, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Walei.
Kongamano hili la siku tano , 4-9 Septemba 2012, lilifunguliwa Jumanne kwa Ibada ya Misa, mjini Yaounde Cameroon , na lina hudhuriwa kwa Wakatoliki walei, wakiwepo pia Makardinali, Maaskofu , Mapadre , na watawa wa kike na kiume. Mkusanyiko huu unaoongozwa na Mada ” Mashahidi wa Yesu Kristu Afrika leo hii: Ninyi ni Chumviya Dunia na Mwanga wa Ulimwengu. Lengo ni kushirikishana uzoefu wa maisha, katiak dunia ya leo, katiak mtazamo wa kuieneja Injili ya Upendo wa Kristu kwa watu wote. RealAudioMP3








All the contents on this site are copyrighted ©.