Tusidhoofishe imani kwa madhulumu ya binadamu – Papa
Jumatano hii ambamo Mama Kanisa ameadhimisha kiliturujia, kumbukumbu ya kifo cha
Yohane Mbatizaji, ambaye pia Siku yake ya kuzaliwa huadhimishwa June 24, Baba Mtakatifu
Benedikto XV1, pia ameiangalisha katekesi yake kwa mahujaji na wageni, juu ya Yohane
Mbatizaji. Kama ilivyokuwa kwa Yohane Mbatizaji, pia sisi Wakristu wa leo, madhulumu
ya binadamu yasidhoofishe imani yetu kwa Kristu. Papa ameizungumzia historia
ya Yohane Mbatizaji ,aliyehubiri ujio wa Kristu , wakati wa Mfalme wa Tiberio kati
ya mwaka 27 hadi 28 AD, akihimiza uongofu wa roho kama hitaji msingi, katika kumpokea
Masiya ajae , Yesu Kristu, Bwana wa Uzima, kama Mwinjlisti Luka alivyoandika, Taz.
Luca 3,4. Papa anasema, Yohane Mbatizaji hakuhubiri tu juu ya maovu na
dhambi, lakini pia alikazia juu ya ujio wa Masiya , Kristu Mkobozi wa dunia, akimwonyesha
Yesu Kristu , kuwa ndiye kweli masiya aliyetumwa na Mungu. Mahubiri hayo ya Yohane
Mbatizaji yaliwezesha, watu wengi kujitokeza kumsikiliza Bwana Yesu, na kumfuata.
Yohane Mbatizaji hata katika madhulumu na shida , aliendelea kuonyesha
uthabiti wa imani yake, hadi maisha yake maisha yake yalipokatishwa kwa kumwaga damu
yake, bila ya upinzani wala kuteteleka. Huu ni upendo wa kweli kwa Bwana wake, upendo
usiochipushwa na ahadi za uongo, na wala vitisho havikuweza kumbadili, maana alikuwa
ametambua njia sahihi ya kufika kwa Mungu. Papa alimalizia na mawaidha
kwamba, tunapokiadhimisha kifo cha Mtakatifu Yohane Mbatizaji, tukumbuke kwamba, pia
sisi Wakristu wa nyakati hizi , tunapaswa kusimama imara katika imani yetu kwa Kristu,
tukidumishwa na upendo wake aminifu wa Iinjili na ushupavu wa kumwachia yote Kristu,
ili akae ndani mwetu, na kuongoza mawazo, nia na utendaji wetu. Na ili
iwe hivyo, muumini tunapaswa kujenga mahusiano ya karibu na Mungu, kupitia matoleo
ya sala na Ibada, silaha kubwa za kuimarisha uhusiano huo. Vipindi vya sala na Ibada
zinapaswa kupewa kipaumbele cha kwanza,kwa kuwa Mungu ndiye mwenye uwezo wote wa kutupa
maisha ya furaha na tulivu, hata katika nyakati za mashinikizo ya kazi na matatizo,
hutuwezesha kuwa mashahidi shupavu wa Kristu. Papa alisali ili Mtakatifu
Yohane Mbatizaji, atuwezeshe pia sisi kuuutambua ukuu na uwezo wa Mungu katika maisha
yetu.