2012-09-12 14:12:09

Maelfu wamzika Kardinali Carlo Maria Martin- Milan


Mapema Jumatatu 3 Septemba 2012, maelfu ya watu waliotajwa kufikia laki mbili, walimiminika katika ukumbi wa Kanisa Kuu la Milan , kutoa heshima zao za mwisho kwa Kardinali Carlo Maria Martini.
Kwa ajili hiyo, Milango ya Ukumbi wa KanisaKuu la Milan, The Doume, iifunguliwa tangu majira ya saa moja za asubuhi hadi saa tano na nusu za asubuhi, ili watu waweze kutoa heshima zao za mwisho kwa Mpendwa wao Kardinali Carlo Martin. Ibada ya wafu na Mazishi , imefanyika katiakkipindi cha alasiri, tangu saa nane na nusu hadi saa kumi mwili wake ulipowekwa kaburini.
Ibada ya Misa ya wafu imeongozwa na Kardinali Angelo Scola, AskofuMkuu wa Milan . Somo la Injili limetoka Injili ya Yohane 6, 37 -44 ambamo Yesu anasema ” wote alionipa Baba watakuja kwangu , nami kamwe sitamtupa nje yeyote anayekuja kwangu . Kwani nimeshuka toka mbinguni si kwa ajili ya kufanya mapenzi yangu ila kutimiza matakwa ya Yule aliyenituma. Na hivyo kila aaminiye atakuwa na uzima wa milele na atafufuka siku ya mwisho".
Mwamzoni mwa Ibada hii, Kardinali Angelo Comastri , Vika mkuu wa Jiji la Vatican na Padre Mkuu wa Kanisa la Kipapa la Mtakatifu Petro la mjini Vatican, alimwakilisha Papa n a alisoma ujumbe wa Papa . Homili ilitolewa na Kardinali Angelo Sodano na mwisho wa Ibada Kardianli Dionigi Tettamanzi , alisoma historia fupi ya maisha ya marehemu.








All the contents on this site are copyrighted ©.