2012-09-12 14:05:16

Maaskofu wapya waanza semina yao ya wiki mbili


Maaskofu wapya wapatao 92, kati yao 63 kutoka Afrika , 17 kutoka Asia na 6 kutoka Amerika ya Kusini na Oceania 6, kwa muda wa wiki mbili , watakuwa na semina yao, katika Chuo cha Kipapa cha Mtakatifu Paulo hapa Roma. Semina hii , iliyoanza Jumatatu hii 3 Septemba inaendelea hadi 15 Septemba 2012 , kama ilivyoandaliwa na Shirika la Kipapa, kwa ajili ya Uinjilishaji wa Watu.
Madhumuni ya semina hii, ni Maaskofu wapya, kupaa ufahamu zaidi juu ya wajibu wa utume wao mpya . Masomo yatatolewa na maofisa mbalimbali na kutoka Idara mbalimbali za Jimbo la Papa. Siku ya Ijumaa , watakutana na Baba Mtakatifu katika makazi yake ya wakati wa kiangazi huko Castel Gandolfo .








All the contents on this site are copyrighted ©.