2012-09-12 14:12:28

Kanisa lawakumbuka wahenga wake Mtakatifu Augostine, na Mtakatifu Monica- Papa


Kwa mujibu wa kalenda ya Kanisa, Jumanne hii, Mama Kanisa amemkumbuka Mtakatifu Augostine Mkuu, ambaye historia ya maisha na uongofu wake , vimeacha utajiri mkubwa wa neema kwa Kanisa.
Jumatatu, ikiwa Siku kuu ya Mtakatifu Monica , mzazi wa Mtakatifu Augostine, Baba Mtakatifu Benedikto XV1, alimtafakari mama huyu, akisema, Mtakatifu Monica kamwe hamtupi mtu wakati wa shida na majaribu, bali huendelea kutoa maombi yake kimyakimya bila kuchoka hadi hapo ushindi unapopatikana dhdi ya mwovu.
Papa anasema, kuonekana kwa furaha za mtu za nje haina maana kwamba hana matatizo yanayomsubua. Kila mtu katika hali ya kibinadamu ana yake yanayomsubua , kama ilivyokuwa kwa Mtakatifu Monica, maisha ya mwanzo ya mwanae Mtakatifu Augustine, yalimsononesha. Lakini kwa neema za imani alizojaliwa Monica, kuwa imani kubwa kwa Kristu, zilisaidia pia mme wake kubatizwa na kufa kifo chema mwaka 371.
Monica aliendelea kutolea machozi ya sala hadi hapo mwanae Augustine , alipoongoka na ubatizwa na kupokea neema za Sakramenti. Uovu unashindwa na sala za mama huyu, ambaye Askofu wa Ippona alisema , Ni vigumu kwa mtoto huyo aliyetolewa machozi mengi kupotelea katika giza la mwovu.
Licha ya shigo ngumu ya mwanae, Monica hakukata tamaa na wala kiburi cha mwovu alichokuwa nacho Augstine, hakiku nyamazisha kilio cha Monica kwa Mwenyezi . Aliendelea kutolea sala , siku hadi siku, hadi alipopata ushindi. Utulivu wa sala, wema na fadhili, zinashida nguvu za mwovu, na kumpa heshima mama huyu ambaye leo hii mfano wa uvumilivu na sala kwa Mama wengi.
Papa ameendelea kumtaja Mtakatifu Monika kuwa mfano na msaada, katika nyakati zetu hizi , ambazo zimejaa maisha ya wasiwasi na hofu itakuwaje siku za usoni. Hali ya maisha yanayo shikiza kujitenga mbali na mwanga , unaoongoza katika furaha kamili ya maisha.
Papa aliendelea kuonya dhidi ya wepesi wa kuona mambo bandia na yenye mpito wa harakaharaka , kuwa ya kuvutia zaidi, lakini kichini chini hujenga hali ya woga, katika kuutafuta ukweli. Woga unaoshinikiza mtu kushindwa kubadili mienendo ya maisha. Katika hali hiyo tunahitaji kudumu katika sala bila kuchoka ili tupate kuuona mwanga unaoelekea katika maisha Matakatifu kama alivyojaliwa Mtakatifu Agostine.








All the contents on this site are copyrighted ©.