2012-09-12 14:04:55

Jimbo Kuu la Mwanza lapata Padre mpya - Celestine Nyanda


Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Jumatano hii limeongeza jina moja zaidi katika orodha ya Mapadre wake , baada ya Shemasi Celestine Nyanda , kula kiapo cha kulitumikia kanisa kwa kuyaishi Matakatifu ya Kipadre.
Padre Mpya , Celestine Nyanda alitoa kiapo hicho katika Ibada ya Misa iliyoongozwa na Mhashamu Askofu Mkuu Yuda Thadei Ruwa’ich wa Jimbo Kuu la Mwanza, na mbele ya waumini waliofika kushuhudia tukio hili.
Askofu Mkuu Ruwaich katika mahubiri yake , alimsisitiza Padre mpya na Mapadre kwa ujumla, kuwa manabii wa kweli kama alivyokuwa Nabii Yeremia. Amesema, wito wa kweli hutoka kw Mungu . Na wito wa kweli ni neema kutoka kwa Mungu. RealAudioMP3








All the contents on this site are copyrighted ©.