2012-09-12 14:12:18

Haitoshi kusikiliza Neno lake tu lakini litekelezeni kwa vitendo ....


Jumapili Baba Mtakatifu Benedikto XV1, akiwahutubia mahujaji na wageni, huko Castel Gandofo, ambako anaendelea na kipindi cha mapumziko ya wakati wa kiangazi , alilenga zaidi katika somo la Injili akisema, somo ni mbiu kuu ya mwaliko kwa watu wote, kuipatanisha imani tunaoihifadhi mioyoni mwetu na utendaji wetu unaoonekana kwa nje. Papa alisali ili neema ya Mungu itutakatifushe ndani na nje ,ili tuweze kuishi kwa kuwajibika kikamilifu katika kutimiza amri ya Kristu na ujumbe wake.
Papa alieleza na kurejea masomo ya Jumapili, yaliyolenga katika amri za Mungu , kipengere muhimu katika maisha ya dini ya Wayahudi na pia kwa Wafuasi wa Kristu ambamo mnapatikana ukamilifu wa upendo wake(taz.Warumi 13,10). Sheria ya Mungu na maneno yake yanayoongoza katika njia ya kweli ya maisha , ambayo inamwondoa mtu katika utumwa wa dhambi na majivuno, na kumwonyesha nchi mpya , huru na yenye uzima tele.
Kwa maana hiyo , sheria zinazotajwa katika Kitabu kitakatifu cha Biblia , si mzigo, au vizingiti au mipaka katia kuyafurahia maisha, bali ni zawadi mwanana ya Bwana, na ni ushuhuda wa upendo wake wa kibaba, unaomweka mtu, kuwa karibu na watu wake. Ni uvuvio ulioinuliwa na kuandika historia ya upendo. Papa alieleza na kurejea maandiko mbalimbali ya Kitabu Kitakatifu cha Biblia, Agano la Kale na Agano jipya.
Homilia ya Papa ilitaja tatizo la nyakati hizi, ni watu kumezwa na kiburi cha kujiona wanajitosheleza katika maisha yao , wakijiwekea sheria na kanuni mpya, na kujenga mwelekeo wa kuzisahau sheria za Mungu na kujitegenezea sheria zinazokumbatia miungu wa kidunia , ufahali na majivuno.
Papa ameasa, sheria ya Mungu hubaki kama ilivyo , hata kama wengine wanaona si muhimu tena katika maisha yao. Na ametahadharisha, Maisha yasiyoongozwa na amri za Mungu, huonekana yenyewe jinsi, mtu huyo anavyotembea njia yenye giza nene , akitafuta njia nyingine huko na kule, akiyumbishwa na sheria za kidunia zinazojaa majivuno na ubinafsi , iwe kama mtu binafsi au kikundi.
Papa anasema hiyo ndiyo sababu ya Kanisa kuingilia kati kwa kuutangaza ukweli kwamba, maisha ya kweli ni kuisikiliza sauti ya Mungu, ni katika kutimiza mapenzi ya Mungu, ambao ni ukweli wa uwepo wako katika maisha mazuri na yenye kuwa na uhuru kamili . Bahati mbaya wengi wanapuuza ukweli huu , kama jambo lisilokuwa na umuhimu , watu wakiridhishwa na mambo ya mpito ya kidunia, yenye kuwaweka mbali na Mungu, na hivyo haisha yao yakijaa hali za wasiwasi na mashaka.
Papa pia ametahadharisha hatari hii ya kuiona dini na mafundisho ya Yesu kuw ani mambo ya kale, lakini kumbe Mafundisho ya Yesu, yaliyoandikwa katiak Injili , ni kwa ajili yetu. Yesu, akihutubia umati wa watu alirejea unabii wa Isaya ” Watu hawana wananiabudu kwa midomo yao lakini roho zao ziko mbali nami. Ninyi mnaiacha amri ya Mungu na kushikilia maagizo ya watu ”Taz. Mc 13,6-7. Na pia Mtume Yakobo katika barua yake, ametahadharisha juuya dini za uongo . Aliwaandikia Wakristu , "Msijidangaye wenyewe kwa kusikiliza tu neno lake , bali litekelezeni kwa vitendo".
Papa alimalizia kwa kumwomba Mama Bikira Maria, asaidie wafuasi wa mwanae, kuifunua mioyo yao wazi na kulisikiliza Neno la Mungu kwa makini na kuiishi kikweli kimawazo na katika utendaji wa kila siku.








All the contents on this site are copyrighted ©.