2018-06-26 16:30:00

Toleo jipya la Mwongozo Katoliki kwa nchi za Mashariki umetolewa !


Katika maadhimisho ya mwaka wa 100 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Kipapa la Makanisa ya mashariki, Limetangazwa toleo jipya la mwongozo Katoliki kwa nchi za Mashariki, na hiyo ni baada ya matoleo mengine ya mwaka   1929, 1932, 1962 na 1974. Kazi ya toleo hiyo inajikita katika mada tatu, na hasa katika kuhusu  Baraza la Makanisa ya Mashariki na toleo hilo limeakilishwa tayari kwenda maduka ya tarehe 15 Juni 2018, kwa kufanya mkutano wa uwakilishwaji  katika  Nyumba Kuu ya Shirika la Wajesuit mjini Roma.

Gazeti la Osservatore Romano wameandika juu ya ujumbe wa  Kardinali Sandri Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki  aliotuoa wakati wa kuwakilisha toleo jipya. Tunawakilisha Kazi ya Kanisa Katoliki la Mashariki, ambalo ni matunda ya hija ndefu na kazi ya kina iliyofanyikwa kwa uangalifu na kwa furaha katika fursa ya maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Kipapa la chi za Mashariki, yeye mwenyewe akiwa ni mwenyekiti wake kusaidia Makanisa katoliki ya mashariki katika dunia.

Sababu nyingi zimetoa chachu kwa Baraza hili kuhamasisha kutengeneza Toleo jipya  la Mashariki katoliki ikiwa ni pamoja na shauku, hawali ya yote kwa waaminikwamba  watambue, watukuze, wapende Makanisa ya Mashariki katika umoja kamili na Vatican Kardinali Sandri aidha amesema, Makanisa Katoliki ya Mashariki yanajulikana kidogo. Tangu enzi za papa Leone II , Kanisa kamili katika makanisa ya Mashariki yalianza kwa taratibu kugunduliwa na daima kuthaminiwa. Ni lazima kutambua zawadi za Makanisa hayo katika Kanisa la Ulimwengu na sadaka kuu ya waamini ambayo walifanya na wanaendelea kufanya kwa upendo  akiwa na umoja kamili na Vatican.  Uwepo wao ni baraka kubwa ambayo inastahili kuthaminiwa vema!

Nchi za Mashariki katoliki zinatakiwa kuwa zawadi kubwa ya Makanisa ya wakristo wa mashariki , wakatoliki, waorthodox na idadi kubwa ya mashahidi na waamini wengi wa imani. Wakristo wa mashariki wanalipa mchango mkubwa kutokana na chuki kwa  kuteswa kwa wakristo au kugawanyika kwao . Ndugu na dada katika Kristo wamelazimika kuhama na wamepoteza kila kitu wakati wa kukimbia kutoka vijiji vyao na ardhi yao asili. Wengi wao wametekwa nyara na kufungwa kwa ajili kukiri Yesu Kristo.

Hata hivyo kwa uaminifu wao katika urithi wa kiliturujia na kitasaufi ambapo wanashirikishana na Makanisa dada ya Kiorthodox , wanaweza makanisa ya mashariki katoliki kuhamasisha umoja kamili unaotamaniwa.  Nchi Mashariki Katoliki ni mchango wa dhati ambao katika mantiki hiyo ni zana inayosaidia waamini wa kiorthodox, wakatoliki , walatini na mashariki , kujitambua wao kwa wao na hatimaye kuwa ndugu kaka na dada wa Baba mmoja na ili ulimwengu upate kuamini (Yh 17,21).

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.