2018-06-23 14:52:00

Uzinduzi wa Jubilei kwa ajili kukumbuka wafiadini 117 nchini Vietnam


Mapema wiki, tarehe 19 Juni 2018 misa kuu tatu zimeadhimishwa ikiwa ni  katika kuzindua rasmi nchini Vietnam Jubileo Maalum ya wafia dini 117 waliotangazwa watakatifu mnamo mwaka 1988 na Mtakatifu Yohane Paulo II. Hao ni mkusanyiko wa mashahidi wa Kanisa wakiwa  watawa wa kike na kiume, wamisionari na walei ambao walipoteza maisha yao wakitetea imani yao  kwa Kristo kati ya  1745 na 1862. Tangu tarehe 19 Juni 1988  hadi 19 Juni 2018 ni miaka 30 imepita na  Kanisa la Vietnam kutoa fursa hii ya hija ya  Jubilei Maalum  ili kufanya kumbukumbu ya kihistoria ya nchi.  Kwa mujibu wa Gazeti l habari za kimisionari Fides linaandika kuwa, maadhimisho hayo yatandelea hadi tarehe 24 Nivemba, siku ambayo Kanisa linaadhimisha sikukuu ya mashahidi 117, ambao walipata kutangzwa wenye heri katika matukio mbalimbali ya mapapa nne kwa mfano: Mashahidi 63 walitangzwa na Papa Leone XIII mnamo mwaka 1900; mashahidi 28 wakatangzwa na Papa Pio X mnamo mwaka 1906 na 1909; mashahidi 25 wakatangazwa na Papa Pio XII mnamo mwaka 1951.

Misa 3 za maadhimisho ya uzinduzi wa Jubilei zimechaguliwa kufanyika katika maeneo msingi  historia ya Kanisa la Vietnam. Ya kwanza katika Kanisa kuu la Mama Yesu Mkingiwa dhambi ya Asili huko Sở Kiện, asili ya mashahidi ndugu wawili Padre Peter Truong Van Thi  na Peter Truong Van Duong. Sehemu ya pili ya misa ilifanyika katika Kituo cha hija cha Mama Yesu wa La Vang, katika wilaya ya Quang Tri, katikati ya nchi, mahali ambapo Bikira Maria aliwatokea baadhi ya waamini wakrisi wakikimbia mateso  miaka 200 iliyopita; na  sehemu ya tatu iliyochaguliwa misa ilifanyika katika kituo cha hija cha Ba Giồng wilaya ya Tiền Giang asili ya maelfu ya mashahidi wa karne ya 18 na 19.

Kuishi tasaufi ya mashahidi kama mashuhuda wa Mungu na Injili ndilo pendekezo la Jubilei Maalum hiyo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Vietnam Askofu Mkuu, Joseph Nguyễn Chí Linh, ambaye pia amewatia moyo waamini wengi ili waweze kuwatembelea watu wenye shida, wagonjwa, wafungwa, wazee, walio na upweke , walemavu kama sehemu kuu ya hija kuelekea kwake Kristo.  Kuhusu mateso ya Wakristo: Maaskofu nane, mapadre 50  walei 59 kati yao akiwa mama mmoja waliouwawa kinyama wanawakilisha kikundi cha mashahidi, lakini wakati huohuo hata sehemu ndogo ya wakristo walioteseka na kuuwawa kwa karne tatu ya kihistoria. Mivutano hiyo ilianza wakati wa ukristo kwenye karne ya XVI ya mwisho wa ufalme wa Nguyễn (1802-1945), aliyeuwa watu wengi kinyama, kwa maana inasadikika zaidi ya wakatoliki 300,000 waliuwawa kinyama. Pamoja na hayo yote leo  hii Kanisa la Vietnam linaendelea kuteseka, lakini kwa kuchota nguvu kutoka na usafi wa mashahidi hao kwa mujibu wa maneno ya Mtakatifu Yohane Paulo II aliyosema tarehe 19 Juni 1988 katika kilele cha kuwatangaza watakatifu.

Anayejulikana sana katika mateso hayo ni Padre Andrea Dũng Lạc, wa Vietnam aliyekatwa kichwa chake mnamo 21 Desemba 1839. Padre Lac alizaliwa mnamo mwaka 1785 katika familia moja maskini ya kivietnam. Akiwa bado mdogo aliuzwa na wazazi wake kwa katekista mmoja mkatoliki, ambaye kwa bahati nzuri alimlea vizuri na akakua kiakili katika akimwelekeza njia ya Kanisa hadi kufikia daraja takatifu la upadre mnamo tarehe 15 Machi 1823. Baada ya kuwa paroko, alipata matatizo makubwa kutoka kwa viongozi watawala mahalia kutokana na ushuhuda wake kwa waamini, hivyo waliamua kumweka mahabusu. Hakutolewa humo hadi waamini kuingilia kati kwa njia ya kulipa fidia. Alihamishwa mara nyingi lakini hali hiyo iliendelea hivyo, kwa sababu ya utume wake wa kufundisha Neno na imani ya Kristo kwa wakatoliki, ndipo waliamua akatwe kichwa chake mara baada ya kulazimishwa kukana imani,akiwa na Padre aliyekuwa amemkaribisha katika parokia yake, Padre  Pietro Trương Văn Thi, ch.

Kanisa la Vietnam pamoja na sifa ya uwepo wa watakatifu wafiadini wengi lakini pia wanafanya ibada kuu ya Mama Maria, hasa katika madhabahu ya La -Vang  kwa sababu ya historia nzuri iliyotokea mnamo mwaka 1798, Mama Maria aliwatokea kikundi cha wakristo wanaoteseka akiwa juu ya mti na kuwaeleza kuwa yeye ni kama mkuu wa mahakama  na “Msaada wa Wakristo”. Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo tarehe 19 Juni 1988 baada ya kuwatangaza watakatifu Mashahidi 117 wa Vietman, wakati wa sala ya Malaika wa Bwana alisema , kutokea kwa Mama Maria wa La-Vang na imani ya mahujaji katika  Madhabahu hiyo, hija ya mawazo yao iwapele moja kwa moja kati ya madhabahu za Mama Maria duniani ili kuweza kutua katika nchi ya Vietnam, nchi yenye rutuba ya damu ya wafia dini 117 ambao wametangazwa”.

Na Sr Angela Rwezaula 
Vaticsn News!
All the contents on this site are copyrighted ©.