2018-06-23 12:00:00

Askofu Norman Wambua ateuliwa kuwa Askofu mpya wa Machakos, Kenya


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Norman King’oo Wambua kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Machakos, nchini Kenya. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Norman King’oo Wambua alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Bungoma. Itakumbukwa kwamba, alizaliwa kunako mwaka 1952 huko Kathian. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 22 Mei 1988. Kunako tarehe 27 Juni 1998, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Bungoma na hatimaye kuwekwa wakfu tarehe 16 Agosti 1998.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.