2018-06-22 13:34:00

Kanisa la Burundi kutetea haki za maisha ya kabila dogo la Batwa !


Kanisa katoliki nchini Burundi linaonesha wasiwasi juu ya hali ya maisha ya kabila la watwa ambao ni kabila dogo lililosahaulika na kuwekwa pembezoni katika umaskini wa kukithiri. Kabila la Batwa linahesabiwa ndiyo wazaliwa wa kwanza kwenye msitu wa kanda za nchi hizo, ambao wanaishi kwa kutegemea kuwinda, kuvua ay kufinyanga wakiwakilisha asilimia 1% ya watu wote wa nchini Burundi ikiwa, asilimia 80 ya kabila la Wahutu na asilimia 15 % ni watusi. 

Sehemu kubwa ya watu wa kabila la Batwa hawajuhi kusoma na kuandika na wanaishi katika nyumba mbovu tu, kwa kuangaikia hata kutafuta chochote cha kujikimu ili wapate kuishi  na haza ile ya kuwinda japokuwa imekuwa na matatizo makubwa katika sehemu kubwa ya misitu kutokana na vita vya wenyeqe kwa wenyewe vilivyo malizika 2005 kati ya makabila mawili makubwa.

Leo hii Burundi inabaki kuwa nchi maskini na ambayo inazidi kuonesha tabia ya mivutano kwa mantiki ya ukosefu wa msimamo wa kisiasa na kiuchumi, lakini pia uliosababishwa na masuala ya ngazi za kimataifa, nchi kushindwa kuheshimu sheria za kidemokrasia za haki za binadamu. Ilikuwa tarehe 7 Oktoba 2016 Makamu wa rais nchini Burundi alitangaza uamuzi wa nchi yake wa kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC). Kwa maana hiyo Burundi ilikuwa ya nchi ya kwanza Afrika   kujitoa  rasmi kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC, tarehe 27 Oktoba 2017 ikiwa ni mwaka mzima baada ya nchi hiyo kuwasilisha risala yake ya kujitoa kwenye mahakama hiyo.

Burundi ilichukua hatua ya kujiondoa kwenye mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ( ICC) kwa hoja kwamba imekuwa ikishughulikia kesi za viongozi wa Afrika pekee na kwamba ilikuwa kama chombo cha nchi za magharibi cha kuzikandamiza nchi za Afrika. Hii ilijiri wakati ripoti kadhaa za mashirika ya kimataifa na hata zile za wataalam wa Umoja wa Mataifa zilikuwa zikipendekeza ICC ianzishe uchunguzi kuhusu makosa ya jinai yaliotokea Burundi jambo ambalo lilitupiliwa mbali na viongozi wa Burundi.

Na ili kuweza kujikita katika dharura ya kibinadamu,shughuli mbalimbali zimewekwa kwenye mchakato na kambi za Kanisa na jumuiya. Kwa namna ya pekee Askofu Joachim Ntahondereye wa jimbo la Muyinga Kaskazini mwa nchi kujikita katika mipango ya kuhamasisha jamii ya Batwa na kuendelea katika shughuli ambazo zilianzishwa na Padre  Fiore D’Alessandri mmisonari wa shirika lwa wasaverian aliyefika mwaka 1966 kuwasaidia maskini kati ya maskini na ambaye aliaga dunia huko Gisanze mwaka 1992.

Shughuli zilizo mstari wa mbele za Kanisa mahaliazinahusu  shule kwa watoto wadodoo na ujenzi wa nyumba ndogo ndogo ili kuwawezesha familia waweze kuondoka katika nyumba za nyasi zilizoko msituni. Shughuli za kimisonari hizo zinafanywa pamoja na wamisionari wa Afrika ambao wametoa kampeni ha mpango wa nyumba ya Batwa, katika kuhakikisha ardhi iweze kutumika kwa ajili ya makumi ya familia na kuwakomboa katoka katika hali mbaya ambayo ni  nusu utumwa ambayo walikuwa wanaishi.

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.