2018-06-13 16:26:00

Matashi mema ya Papa katika kuwania Kombe la Dunia Urusi 2018!


Kesho unafunguliwa  mechi ya Kombe la Dunia nchini Urusi. Ni shauku yangu kuwatumia salam zangu wachezaji wote na waandaaaji kama  hata, wale washabiki ambao watatazama  mpira kupitia vyombo vya habari katika tukio hili linaloshinda kila aina ya mipaka.
Ni matashi mema  ya Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya katekesi yake Jumatano 13 Juni 2018  kwa mahujaji na waamini katika viwanja vya Mtakatifu Petro mjini Vatican. Baba Mtakatifu amesisitiza kwamba, tukio hili muhimu la michezo linaweza kuwa fursa ya makutano, mazungumzo na undugu kati ya tamaduni na dini tofauti kwa kuimarisha mshikamano na amani kati ya nchi.

Halikadhalia salam zake zimewaendea waliofika hapo na zaidi kama alivyo anza katekesi yake mwanzo kukumbuka sikukuu ya Mtakatifu Antoni wa Padova, Mwalimu wa Kanisa na msimamizi wa maskini. Amesema Mtakatifu Antoni anatufundisha uzuri wa upendo wa kweli na wa kujitoa bure, aidha kwa vijana, wazee wagonjwa na wanandoa wapya amesema ni katika kupenda  kama Yeye alivyo penda, ndipo unaweza kuhisi kutokuwekwa pembeni na kupata nguvu zaidi ya kushinda majaribu ya maisha.

Hata hivyo kuhusiana na mechi ya kuwania kombe, yamebakia masaa machache kuelekea kwenye michuano ya kombe la dunia itakayofanyika nchini Urusi, na TELESTAR ni mpira ambao utatumika kuelekea kwenye fainali za kombe la dunia. Mpira huo umetengenezwa na kampuni ya Ujerumani, ambayo inatengeneza vifaa vya michezo vya Adidas. Mpira wa aina hiyo ulianza kutengenezwa tangu mwaka 1970, na kupewa jina la Telestar na ulitumika katika fainali iliyofanyika nchini Mexico.Una uwezo mkubwa wa wepesi kuruka angani kwa kiasi kikubwa.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News
All the contents on this site are copyrighted ©.