2018-06-12 15:52:00

Papa anasema,ushuhuda wa mkristo ni kuwa chumvi na mwanga kwa wengine!


Chumvi inasaidia kutoa radha ya chakula na mwanga hauwezi kujiangaza pekee yake, kwa namna hiyo ushuhuda rahisi wa mkristo wa kila siku unawasaidia wengine na si kwa sifa binafsi, bali kwa ajili ya utukufu wa Mungu baba. Ni tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko siku ya Jumanne, 12 Juni 2018 aliyoitoa wakati wa maadhimisho ya Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta Mjini Vatican. Akifafanua zaidi amesema, ni kuwa chumvi na mwanga kwa ajili ya wengine bila kujisifia. Na ndiyo jambo rahisi la ushuhuda wa kawaida, yaani utakatifu wa kila siku ambao kama mkristo amealikwa kuutafuta.

Katika mahubiri yake kupitia Injili ya Siku, Baba Mtakatifu anathibitisha, ushuhuda mkubwa wa mkristo ni ule wa kujitoa maisha kama Yesu alivyo fanya, yaani kuwa shahidi lakini kuna jambo pia kubwa la ushuhuda wa kila siku ambao unaanzia asubuhi, mara baada ya kuamka hadi  jioni na wakati wa kwenda kulala. Hata hivyo anaongeza kusema, ndiyo, yote inawezekana kufikiriwa jambo dogo lakini kwa Bwana kila jambo dogo tufanyalo ni muujiza, na kushangaza, ndiyo maana lazima kuwa na tabia hiyo ya unyenyekevu ambao unahusiana kutafuta namna ya  kuwa chumvi na mwanga tu.

Ni kuwa chumvi na mwanga kwa ajili ya wengine kwakuwa chumvi haitoi radha peke yake, kwa maana daima ni katika kuhudumia. Vilvile hata mwanga hauonekani ka siyo katika huduma. Chumvi ni kidogo inayosaidia kuleta radha katika chakula maana ni chumvi kwa ajili ya wengine. Akitoa mfano zaidi, amesema, sokoni kwa kawaida hawauzi tani ya chumvi, bali chumvi imefungwa katika mifuko midogo midogo na inatosha! Na chumvi haiwezi kujivunia peke yake sababu haijisaidii. Daima ni kusaidia wangine, husaidia kuhifadhi mambo na kuleta radha ya mambo na ndiyo maana ya ushuhuda, amethibitisha!

Kuwa mkristo wa kila siku ina maana ya kuwa kama mwanga, kwa ajili ya wengine na kuwasaidia wakati wa giza. Baba Mtakatifu ametoa mfano mwepesi wa kutambua vema juu ya kazi ya mwanga na chumvi na kusema: hata Bwana anasema “wewe ni chumvi na mwanga, ni kweli. Lakini usifikiri utavuta watu wengi Kanisani. Hapana, bali, utafanya watu waone na kumsifu Baba na vilevile hautapewi sifa yoyote. Hioyo ni sawa sawa na tunapokula chakula mezani, hatusema kuna chumvi nzuri, badala yake tunasema, chakula ni  kizuri na nyama tamu. Halikadhalika tunapokuwa tunakwanda nyumbani usiku, hatusemi kuna mwanga mzuri” kwa maana  tunaudharau mwanga huo; Ni kwa kuwa  tunauishi mwanga huo unaoangaza!

Utakatifu wa kila siku: Sisi siyo hatuko mstari wa mbele kujisifia binafsi, amesititza Baba Mtakatifu na siyo lazama kufanya kama mfalisayo ambaye alimshukuru Bwana akifikiri yeye ni mtakatifu. Kwa maana hiyo ingekuwa vizuri kufanya tafakari zaidi mwisho wa siku kwa kujiuliza; je leo nimekuwa chumvi na mwanga. Huo ndiyo utakatifu wa kila siku na Bwana atusaidie kutambua jambo hilo, amehitimisha Baba Mtakatifu Francisko tafakari yake ya siku.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.