2018-06-12 16:18:00

Mkutano wa Familia Duniani ni fursa ya kuadhimisha na kusaidia familia!


Mkutano Mkuu wa tisa wa Familia Duniani utakuwa ni fursa ya kuadhimisha, kuthibitisha, kutambua na kusaidia familia. Haya yametamkwa na Askofu Mkuu Wamon Martin , Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Ireland  kwa vyombo vya habari huko Maynooth tarehe 11 Juni 2018, wakati akielezea ratiba rasmi ya Ziara ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko. Akiendelea amesema, Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 25-26 Agosti itakuwa ni hitimisho la Kongamano la Kitume ambalo linaandaza tarehe 21 Agosti. Katika program,iliyoandaliwa na kuongozwa na familia, walei inatarajiwa kuwapo  watoa mada na ushuhuda watu 200 kutoka mabara matano ikiwa ni pamoja na ( wanawake 91 , wanaume 65, mapadre na watawa 44. Waraka wa Baba Mtakatifu Francisko wa Amoris Laetitia- Furaha ya upendo ndani ya familia ndiyo mada kiongozi katika kongamano hilo, mahali ambapo watajikita kwa undani kutafakari changamoto ambazo leo hii familia inakabiliana nayo, kama vile umaskini, madawa ya kulevya manyanyaso katika familia, talaka za ndoa, uhusiano wa jamii za mashoga (Lgbt) mambo ambayo ni hali halisia katika familia ya sasa inakabiliana nayo. Amesisitiza Askofu Mkuu Eamon Martin.

Hata hivyo kati ya mada hizo bado kuna hata mchakato wa maandalizi ya kufunga ndoa, urithishwaji wa imani, mshikamano kati ya kizazi, masuala ya teknolojia mpya, nafasi ya familia katika utunzaji na ulinzi wa mazimgiria, wito wa kuwa baba leo hii.  Kadhalika amesema, hadi sasa watu ambao wamekwisha jiorodhesha katika tukio hili ni  karibia 30,000, ambayo ni namba kubwa kuwahi kutokea tangu kuanzishwa kwa Siku ya familia duniani; karibia watu 6,000 chini ya miaka 18 na 11,000 kutoka nchi za nje ambazo ni nchi 103. Wananafamilia waliojiandikisha ni kati ya umeri kuanzia miaka 29 na 40. Na watu waliojiandikisha  kujitolea ni 5,500 ili kusaidia watu katika tukio hili.
 
Ikumbukwe subira na shauku kubwa ya kusibiriwa Baba Mtakatifu Francisko katika sikukuu ya familia mahali ambapo Siku ya Jumamosi jioni ya tarehe 25 Agosti ataungana na familia kufanya sherehe, wakati huo Jumapoli 26 Agosti katika Uwanja mkubwa wa Phoenis ataadhimisha Misa Takatifu ya kufunga Siku hiyo maalum ya Familia duniani.  Askofu Mkuu Martin akiendelea na habari kwa wandishi wa habari amesema, Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko si tukio moja tu la kawaida, kwa maana anafika katika kipindi ambacho Kanisa la Ireland linapambana ili kupata nafasi katika jamii na utamaduni wa Ireland, ile nafasi tofauti na ilivyo sasa, yaani kurudi katika nafasi uliyokuwa inatawala nchi ya Ireland wakati uliopita. Baba Mtakatifu ni mtu anayejionesha katika ulimwengu ambao utafikiri imani imewekwa pembeni, kwa maana hiyo  katika maadhimisho haya, inawezekana kuishi na kuguswa mioyo ya watu na kuchangamotisha ili watafakari na kuchagua thamani msingi ya  maisha kwa ajili ya jamii.

Askofu Martin aidha amesema, Baba Mtakatifu Francisko anatafuta njia za kuweza kurudisha kwa hali na mali, Moyo wa mafundisho ya Yesu, bila kulazimisha au kuhukumu, badala yake kuvutia kwa urahisi kutokana na mifano halisi ya maisha. Aidha amesema, Baba Mtakatifu Francisko anafikiria mkutano wa familia si kama zawadi ya kumbukumbu kwa ajili yetu sisi, badala yake ni zawadi ambayo Kanisa la Ireland linaweza kushirikishana na wengine. Na hivyo amehimimisha akiwa na matumaini  kwamba  mkutano wa familia duniani nchini Ireland, unaweza kuhitimishwa, wakati huo huo, ukiwa umepyaisha, umevutia, matumaini, na zaidi kuponyesha.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.