2018-06-08 12:32:00

Viongozi wa dini nchini Myanmar wamemaliza Jukwaa kuhusu dini ya amani !


Wakati endelevu wa nchi ya Myanmar umesimamia  juu ya utajiri wa historia na utamaduni wa kuishi kwa pamoja kama madhehebu na tamaduni nyingi. Kwa ngazi ya kina, hiyo inatoa ahadi ya wakati endelevu kwa uhakika wa thamani na fadhila ya huruma, ustawi wa kushirikishana na haki iliyopo katika utamaduni mkuu wa dini za nchi ya Myanmar. Huo ndiyo uthibitisho wa Waraka wa viongozi wa dini Barani Asia kwenye Jukwaa la Dini kwa ajili ya Amani, lililo malizika hivi karibuni kwa  kuongozwa na Kardinali Charles Maung Bo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki la Yangon.

Ujumbe umewafikia kwa Barua maalumu watu wote na wenye mapenzi mema wan chi ya Myanmar. Katika waraka wao, unasomeka kwamba, viongozi wa wabudha, wakristo, wahindu na waislamu wa Mynamar na kanda yote wanaandika kwa ushirikiano na matumaini ya amani. Aidha wanaonesha katika waraka huo, wameunganika katika kipindi kigumu ambacho kinataka kutazama kwa kina nchi yao. Kwa kuzingatia juhudi zao nyingi za wanaume na wanawake, amabo wameweza kushinda mateso na kuponyesha majeraha ya wakati uliopita. Nchi ya Myanmar imejionesha duniani kuwa, inawezakana kipindi cha mpito wa amani yaani kutoka katika serikali za nguvu namabavu.

Aidha  waraka  wa viongozi wa kidini wanakumbusha hata kupindi cha majanga ya hali ya hewa  yaliyotokea huko Nargis mwaka 2008,ambapo  wamonaki wa Kibudha waliokoa watu wengi walio athirika katika vijiji. Mashiriika ya kikristo ya kibinadamu walitoa mchango mkubwa wa kutoa msaada kwa wale wote waliokuwa wanateseka; wahindu, waislamu na makundi mengi waliunganika kwa pamoja kusaidia ndugu zao. Huduma na maisha ya pamoja ndivyo vitu vyenye thamani msingi wa  watu wa Myanmar na umoja katika utofauti ni nguvu ya nchi hiyo wanasthibitisha!

Hata hivyo pia pia viongozi wa kidini wanahimiza juu ya kupinga tabia za kujipendelea kwa dini au kabila katika kushirikiana na watu wote, kwa maana hiyo wanajitahidi kutoa mchango wa kuweza kutoa suluhisho la migogoro ya kijumuiya ili kuweza kuendelea na mapatano ya kitaifa , kwa namna hiyo wanaomba sala ya amani ili kuongeza nguvu ili kuondokana na kipindi cha mpito wa udikteta kufika demokrasia ya kweli , kama vile kuondokana na migogoro ili kuwa na amani kamili. Waraka pia unashutumu vikali juu ya chuki katika mitandao ya kijamii inayokiuka misingi ya kiroho hasa katika uvumilivu na heshima. Viongozi wa kidini wanaitaka serikali iwajibike kwa dhati ili kuhakikisha amani na ustawi wa watu ambao wamo pembezoni mwa jamii hasa wakitazama watu wanaoishi katika serikali ya Rakhine.

Katika suala la hali huyo wanawaalika hata Umoja wa mataifa kurahisisha mchakato kwa ajili ya maisha na amani, mendeleo, elimu, na haki ya kibindamu kwa ajili ya jumuiya ya Serikali ya Rakhine, wakiwa na matumaini makubwa ya kuwa mwafaka unaweza kupatikana wenye msingi wa hadhi ya binadamu na ustawi wa kushirikishana. Na maisha endelevu ya watu wa Myanmar yako katika maombi yao wote!

Na Sr Angela 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.