2018-06-07 13:43:00

Ujumbe wa mwisho Baraza la Makanisa Ulaya kutaka kuwa wajenzi wa madaraja!


Tutajitahidi kuwa wajenzi wa madaraja kwa uwezo wa mabadiliko ya imani na kwa uwajibu wa upyaisho katika mambo matatu: ushuhuda, haki na kukaribisha. Ni ahadi ya utume wa Kanisa la Ulaya na Makanisa yote ya kikristo yaliyomo katika bara hilo, waliyopendekeza kuifanya mara baada ya siku 9 za kujikita katika mkutano wao wakikabiliana na mada za changamoto ambazo Bara la Ulaya linapitia nyakati hizi. Ujumbe wa mwisho wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Ulaya (CEC ) ulio fanyika huko Novi Sad nchini Serbia kuanzia tarehe 30 Mei hadi 7 Juni 2018, umejikita katika mambo msingi  na hasa kwa ajili ya utekelezaji  thabiti. Mkutano ulioudhuriwa na wawakilishi 450 kutoka Makanisa tofauti 116, ambapo ujumbe unaonesha nia kweli ya kuunganika kwao katika kipindi cha kuyumba  kwa bara la Ulaya.

Barani Ulaya ni mahali ambapo watu wengi wanafanya uzoefu wa kupoteza hadhi, unyanyasaji, umaskini na utumiaji vibaya wa madaraka. Kwa maana hiyo ujumbe unasisitiza kwamba, kutoka mto ya Danubio hadi Novi Sad, mahali ambapo madaraja yalikuwa yamewaharibiwa wakati wa migogoro na kujengwa upya kwa amani, wao wameungana kutafakari na maombi. Wameshirikishana kiu zao za haki; wasiwasi wakina  kwa ajili ya watu wao, kwa ajili ya bara lao  hata kwa dunia nzima. Kadhalika wanasema, kushuhudia Kristo lehi hii Barani Ulaya, maana yake ni kuwa familia moja, kwani kila mtu ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu; kwa kuthamanisha sauti ya vijana ambao ndiyo wakati uliopo na endelevu wa Bara la Ulaya. 

Na ili kuweza kujikita katika matendo  ya dhati ya haki, wanaomba taasisi zote za Serikali  na makanisa kufanya kazi kwa pamoja ili vurugu ziweze kusitishwa, mateso na ubaguzi, kutetea na  uhuru wa dini na imani. Aidha ina maana ya kutafuta mapatano na suluhisho la amani katika migogoro; kujikita katika kusikiliza wale ambao hawana sauti au wanajikuta pembezoni mwa Makanisa, jumuiya na katika dunia nzima. Mwisho Makanisa hayo yanathibitisha juu ya wajibu wao hasa katika kukaribisha, kutoa kwa dhati ukarimu kwa  wakimbizi na wageni wote, dini au imani, zaidi katika mazungumzo, kushirikishana na imani za kikristo; kujifunza kupitia  mmoja na mwingine, kutoa mchango katika  kushinda vikwazo vya utengano na ubaguzi, ili kuweza kuhamasisha hali halisi ya kutetea hadhi za binadamu!

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

 
All the contents on this site are copyrighted ©.