2018-06-07 14:30:00

Kard.Mteule Coutts:Mazungumzo ya maisha na huduma ya binadamu mteswa!


Mazungumzo ya kidini ni shughuli ambazo wanapaswa kuhusika wote na hasa ulazima kufanya  sehemu ya ushirikishwaji katika maisha  na kama ilivyo sehemu kubwa nchini Pakistan watu  ni waislam. Ndiyo matashi mema ya Kardinali Joseph Coutts ambaye tarehe 28 Juni 2018, atasimikwa rasmi kwa kupewa kofia mpya  ya ukardinali wakati wa maadhimisho ya Makardinali na  Baba Mtakatifu Francisko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Katika mji wa Karachi ambao ni moja ya miji mikuu duniani yenye wingi wa watu kati ya milioni 19 na 21 , wanaishi jumuiya kubwa ya kihindu na wakristo. Kardinali Mteula ameeleza kwamba, nchi hiyo ni jamii yanye utajiri wa  utamaduni mwingi na dini nyingi pamoja laikini pamoja na dini hizo  bado kuna dini ya  Bahai, Parsi na badhi ya Wasikh. Amethibisha pia kuwa kati ya vikundi vya kwanza vya dini vilivyofika kumtakia matashi mema mara baada ya kuteuliwa kuwa Kardinali ni kikundi cha viongozi  15-20 wa jumuiya mbalimbali, kwa njia hiyo ni muhimu  kuishi, kushirikiana na kupongezana kama ndugu wamoja !

Shirika la habari za kimisionari Fides limesema, Karidinali mteule hivi karibuni ameona jinis gani kuna ongezeko la makundi ya itikadi kali ambao wanatumia dini kudharau na kunyanyasa wengine. Kwa maana hiyo anathibitisha kuwa, hali hii ni ya dharura ya mazungumzo ya dhati zaidi ya maneno, ni mazungumzo ya maisha, ili kuweza  kukubaliana na mwingine, kujifunza kumtambua na kumpokea mwingine, kufanya kazi kwa pamoja na umoja. Pamoja na hayo anasema hali hii pia ilikuwa tayari imezungumzwa na katika Mtaguso wa II wa Vatican kwenye Waraka wa (Nostra Aetate) ambao ulikijita kutafakari kwa kina suala hilo, kwa maana hiyo kama Kanisa halipaswi kujifungia binafsi, badala yake ni kutoka nje na kukutana wengine.
Kardinali amethibitsha pia, kwasasa wanaishi katika dunia ya kisasa, na hivyo wanao wajibu mkubwa kufanya kazi na madhehebu mengine ya kidini  na hasa katika kutazama umuhimu wa thamani chanya zilizomo kwa kila utamaduni na dhehebu, kwa namna ya kudumisha kile kinacho waunganisha zaidi ya kile kinacho watengenisha. Katika mazungumzo mambo hayo msingi hujitokeza, maana. Hata viongozi wa serikali  wanazungumza mahitaji ya kuhamasisha umoja wa kidini na wa kijamii daima. Kardinali mteuli Coutts anahitimisha akionesha imani aliyo katika umuhimu wa mazungumzo ya maisha zaidi maneno matupu tu. Kwa maana hiyo anasema, ipo dharura ya kufanya kazi pamoja juu ya thamani ya pamoja.

Kwa upande huo, amekumbusha baadhi ya watu mashuhuri au wahanga wa nchi yao, kama vile mwislam Abdul Sattar Edhi aliyekufa miaka kadhaa iliyopita. Alikuwa amejikita katika juhudi za mshikamano kijamii bila kujali dini yoyote, badala yake aliongozwa na msingi wa upendo wa kibinadamu. Mfano mwingine ni ule wa dada mkristo Ruth Pfau, ambaye alifanya kazi katika utume na wagonjwa wa ukoma. Wote wawili wamekuwa mfano wa kuigwa katika huduma ya binadamu anayeteseka, na wanastahili kuheshimiwa na kutazamwa kwa macho ya watu na serikali. Ni mifano miwili ya watu ambao kwa nchi ya Pakistani wamejenga madaraja na kubomoa kuta za ubaguzi, chuki na vurugu.

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News
All the contents on this site are copyrighted ©.