2018-06-07 14:45:00

Askofu Borwah wa Liberia:Zipo changamoto za nchi lakini inahitajika muda!


Rais mpya George Weah alichanguliwa na vijana waliokuwa wanahisi kubaguliwa na kuwekwa pemebezno mwa jamii na viongozi wa kitaifa  kwa mujibu wa Askofu Mkuu Anthony Fallah Borwah, wa Jimbo Kuu Gbarnga  na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu  wa Liberia, akizungumza na Shirika la habari za kimisionari Fides wakati  wa kutazamia kufanya hija ya kitume ijayo mjini Vatican.

Askofu Borwah amesema, Rais George Weah anawakilisha historia ya mafanikio kwa kizazi cha vijana, Alichanguliwa miezi sita iliyopita, lakini kwa kipindi kifupi  ambacho kwake  kilikuwa kigumu amejifunza kufanya urais kwa namna ya haraka japokuwa lakini, watu hawana uvumilivu, maana wameisha anza tayari kulalamika.  Hiyo lakini inahitaji kuwaeleza watu hasa vijana kwamba, Rais mpya nayE   anahitaji muda ili kuweza kuona matokeo ya dhati.

Rais Mpya Weah wa Liberia alishinda uchaguzi tarehe 26 Desemba 2018. Kama Kanisa wanatafuta kimsaidia Rais huyo lakini Askofu Borwah amesema kati ya mambo mengi, nafasi ya kwanza ni ile ya umaskini na ukosefu wa ajira unao wakumba sehemu kubwa ya watu. Hali halisi ya uchumi ni mabaya sana, hata kutokana na matokeo ya mlipuko wa Ebola ambayo iliwapigisha magoti nchi kwa upande wa kiuchumi.  Mahangaiko hayo kwa vijana wengi, ndiyo iliwafanya kuona sura ya George Weah  kama mmoja wa kuleta  matumaini ya wakati hujao, japokuwa bado inahitaji muda wa lazima katika utekelezaji wa kazi.

Licha ya hayo yote pia Askofu anaamini kuwa Rais Weah, lazima achague timu nzuri ya serikali itakayo msaidia. Hiyo ni kwa sababu kwa kipindi kidogo tu cha miezi michache  wameona matatizo katika baadhi ya watu ambao amewachagua katika serikali kuwa karibu kumsaidia lakini wenye ukosefu wa maandalizi na ujuzi. Ndiyo Rais anataka kuwapa nafasi vijana katika serikali, ni shauku inayotambuliwa na wengi, lakini huwezi kuunda timu katika serikali yenye vijana tu wenye ari na shauku bila kuwa na ujuzi wa kukabiliana na changamoto za mbele, ni lazima kufanya serikali mchanganyiko, wa vijana na watu wazima wenye ujuzi, utaalam na busara na waliokomaa katika masuala ya kisiasa, kwa upande wa maskofu wanashauri. Rais wa nchi anahitaji kuwa na hekima kubwa ya kung’amua na kuchagua timu yake makini. Na kwa maana hiyo amerudia kusema kwamba, kama Kanisa wako tayari kufanya kazi pamoja na serikali ili kutoa ushauri kwa ajili ya wema wa nchi.

Kwa upande mwingine Askofu Borwah amethibitisha kwamba, Rais Weah  anajitahidi. Ni mtu mwenye mpango wa kisiasa  ulio bora ambao  unakwenda sambamaba na Mafundisho jamii ya  Kanisa hasa ya kujikita katika kutoa kipaumbele zaidi cha maskini kama jiwe la waashi lililowekwa pembeni. Hali ya Kanisa katoliki  la Liberia kwa mujibu wa Askofu Borwah, amesema wapo Maaskofu watatu tu ambao pamoja na umaskini na matatizo mbalimbali yaliyopo wanajitahidi kufanya kazi kwa pamoja na umoja. Iwapo waamini wanatazama wachungaji wao wameunganika kwa pamoja, watawafuata. Kama maaskofu kwa sasa wanatoa mfano wa umoja, mapatano na amani katika nchi ambayo imejaribiwa kwa muda mrefu na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyo malizika 2003.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

 
All the contents on this site are copyrighted ©.