2018-06-06 14:24:00

Wakatoliki nchini Cameroon wanataka amani ya kweli dhidi ya mivutano


Mivutano ni kama vile visu vina katakata na hata kama mijini  hakuna mapigano, lakini wafanyabiashara wa maduka na  wale wadogo wadogo  wanaogopa kuharibiwa shughuli zao  na kuwaletea hasara. Waendesha Tax katika miji pia wanaogopa kushambuliwa. Mji umegeuka kama umechemshwa maji ya moto. Huu ndiyo uthibitisho wa ushuhuda wa mmisionari Mkapuchini, ndugu Gioacchino Catanzaro akielezea hali halisi ya hofu na mivutano iliyopo katika mji wa Bamenda, mji ambao ndiyo msingi wa lugha ya kingereza nchini Cameroon. Kwa maana ni miaka sasa katika kanda zilizoko Kusini Mashariki na Kaskazini Mashariki ya nchi, wanahisi kubaguliwa na serikali ya Kati.

Wakameruni wanaotumia lugha ya kingereza wanadai viongozi wa Yaunde kuwalazimisha kutumia  lugha na tamaduni za kifaransa katika mahakama, ofisi za umma na mashuleni. Kwa miaka mingi wilaya za lugha ya kingereza wamekuwa wakiomba kupewa nafasi kubwa kwa ajili ya kutumia utumaduni wao japokuwa kwa sasa wameweza kuupata, lakini ambao siyo dhabiti kufatia na mivutano inayoendelea hadi sasa. Tangu 2016 maandamano makubwa yamekuwa yakifanyika ya kudai uhuru. Tarehe 1 Oktoba 2017 majimbo hayo makubwa yaweza kujitangazia uhuru wa majimbo mawili ya lugha ya kingereza huko Cameroon na kuzaa Jamhuri ya Ambazoni. Tendo hili limesababisha mivutano ambayo haijawahi kusikika katika majimbo hayo mawili. Kwani bado kuendelea na mapigano makali kati ya wadai uhuru na nguvu za kiselikali na mamia ya watu wamekufa na wengine kujeruhiwa.
 
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa zaidi ya watu wa Camerroni 160,000 wameacha nyumba zao ili kutafuta usalama katika sehemu nyingine za nchi yao au nje ya nchi hasa Nigeria. Sehemu kubwa ya wahamiaji kwa mujibu wa Ripoti ya Umoja wa mataifa, wanaishi katika misitu. Hata hivyo, hivi karibuni mbele ya migogoro hiyo ya kijamii, hata  Maskofu wa Cameroon wemetoa wito kwa ajili ya kipeo hicho cha nchi, wakiomba ufunguzi wa milango ya mazungumzo ya kweli kati yao, ili kuweze kuondokana na kipeo hicho cha vita ambacho wanathibitisha hakina maana na wala msingi.

Padre Gioachino akiendelea na  ushuhuda katika vyombo vya habari za kimisionari Fides, amesema, katika nyakati hizi huko Bamenda hakuna mapigano barabarani, japokuwa wasiwasi ni mkubwa hasa kwa sababu watu wote wanahisi hali ya kivita inayoweza kulipuka wakati wowote. Maisha ya kijamii kwa sasa yamegeuka kuwa ya bure, kwa maana miezi iliyopita shughuli mbalimbali za watu zilishambuliwa na kuchomwa moto. Wafanya biashara na zile ndogo ndogo walifunga shughuli zao. Wafanya biashara katika maduka makubwa wamefunga, kwa maana hiyo, hata kupata mfuko wa simenti inakuwa shida kubwa.

Na Sr Angela Rwezaula
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.