2018-06-06 14:41:00

Semina ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Kanda ya maziwa makubwa


Hivi karibuni mjini Kinshasa imemalizika semina ya siku mbili ambayo ilikuwa na matunda ya kutafakari na kubadilishana utendeji wa shughuli zao za kitume, iliyoandaliwa na Shirikisho la Mabaraza ya Maakofu wa Kanda ya Afrika ya kati (Aceac) iliyofanyika mjini Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Aliyefungua Semina hiyo alikuwa ni Askofu Mkuu wa Kisangani, Marcel Utembi Tapa ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Congo, kwa kusititiza umuhimu wa mkutano huo kwamba, hawali ya yote ilikuwa ni kuweza kuweka malengo thabiti ya mkakati na matendo yaliyo mstari wa mbele, udhati wa utume wa ushirikiano na ubunifu uliokabidhiwa na seketrarieti kuu ya Shirikisho la Mabaraza ya maaskofu wa Afrika ya Kati (Aceac katika kanda za maziwa makuu.

Washiriki wa semina hiyo karibia ishirini walikuwa wakiwakilisha nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, Burundi na Rwanda, pamoja na wajumbe kutoka Caritas internationalis mahalia na baadhi kutoka nchi za Ulaya na mashirika ya Kanisa na kibinadamu. Askofu Mkuu Utembi ametoa shukrani kubwa kwa wote waliofika katika kazi hiyo na  yenye thamani, ambayo imeleta matokeo mema ya muungano wa Makanisa ya Afrika ya kati  na kusaidia mipango yenye msingi na mantiki ya huduma ya upendo kwa kuzingatia kuwa, kanda ya maziwa makubwa imekuwa ikipitia kipindi cha joto la kisiasa na kijamii ambapo watu wasio kuwa na mtetezi, wala ulinzi bado wanahisi kuachwa peke yao

Hata hivyo pia  Mkakati wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika ya kati (Aceac) unatazamia kuingilia kati katika mapambano ya umaskini,utunzaji wa mazingira, mazungumzo ya tamaduni, kama vile ushirikishwaji wa pamoja kati ya utofauti za  utamaduni, dini, lugha.

 Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

 
All the contents on this site are copyrighted ©.