2018-06-06 14:58:00

Mwelekeo wa mtindo mpya wa maisha na uwajibikaji katika ulinzi wa mazingira


Changamoto hazitazami mambo ya kiuchumi na kisiasa tu, bali hata mtazamo wa kichungaji ili kuufanya uweze kupatikana  katika majukumu ya mshikamano na udhaifu wa mazingira mbele ya uso wa athari za mababadiliko ya sasa katika mtazamo wa huduma kamili. Inahitaji kupatikana ule uhusiano  kati ya hutoaji huduma kwenye  maeneo yote na ule wa watu,wakati huo huo, kuwa na mwelekeo wa maisha mapya katika matumizi na  uwajibu, ikiwa ni  pamoja na kufanya uchaguzi  wa kudumu kwa upande wa jumuiya nzima kwa ajili ya maendeleo ya jamii kwa ujumla.  Huo ndiyo uthibitisho wa Ujumbe wa Baraza la maaskofu wa Italia (Cei) Katika Siku ya 13 ya Madhimisho ya utunzaji wa Mazingira, itakayofanyika mnamo tarehe  1 Septemba 2018, ujumbe wao unaongozwa na  kauli mbiu: Kukuza agano na dunia. 

Ujumbe unaendelea kueleza kwamba, shughuli mbalimbali zilizoanzishwa kwa maana ya kijimbo na vyama vya Kanisa kama vile vya kiekolojia ni umuhimu kwa kampeni ya kuweza kupata uhuru kamili kutoka kwenye vyanzo vya nishati mbadala au vigezo vingine vingi vya jumuiya kwa kuishi ule uongofu wa mazingira, lakini pamoja na hayo yote  kuna mtazamo wa kukuza roho, kama asemavyo Baba Mtakatifu Francisko kwamba: ni muhimu kutoa msingi kwa tahadhari hiyo, kwa kujikita kwa utaratibu katika kozi za mafunzo kwa wote wanao husika katika jumuiya ya Kanisa. Ujumbe  uliotolewa na Gazeti la Avvenire la Baraza la Maaskofu Katoliki la Italia, umetiwa sahini na Tume ya Baraza la Maaskofu kwa ajili ya matatizo ya kijamii, kazi ya haki, na amani, na Tume ya Baraza la maaskofu kwa ajili ya uekemene na mazungumzo ya kidini.

Kadhalika ujumbe umeandikwa: “Mara kwa mara ardhi yetu, vijiji, na miji mikubwa imeharibiwa na matukio ya anga zaidi kuliko yale tuliyokuwa tumezoea kuyaona ya kawaida, na wala mabadiliko ya hali ya hewa sasa si tishio tu linalohusishwa na mgogoro wa kijamii na mazingira kando yake pia ni kufikiria pia uchafuzi wa mazingira unaoenea na matukio ambayo wakati mwingine huletwa na suala hilo! Mtazamo wao na wasiwasi pia ni juu ya sayari hii kutokana na ongezeko la joto , ambapo wanaeleza jinsi gani kuna ulazima wa kulinda miji na maeneo yote hasa katika kukabiliana na changamoto hiyo kwa vipimo vinavyotakiwa, na si kinadhalia bali mantendo hai.

Hata hivyo kutokana na mabadiliko hayo mkutano mwingine wa Kimataifa COP24 utafanyika huko Katowicze Poland mwezi Desemba 2018: katika tukio hilo  ni kwa ajili ya kufikiria na kujikita kwa kina juu ya kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yalianza mkakati wa miaka mitatu kufuatia na ule wa COP 21 uliofanyika huko Paris nchini Ufaransa; pia kutakuwa na uwezekano wa kuhamasisha kazi ya hadhi na umakini wa nguvu kwa ajili ya mazingira, wakitafakari maelekezo ya Wiki ya Kijamii iliyofanyika huko Cagliari 2017 nchini Italia. Kwa njia hiyo ujumbe unasema, Utume wa kibinadamu unaokuza ardhi hauwezeikwenda kinyume na ile hatua ya kulinda ardhi hiyo.

Katika ujumbe huo pia unaonesha wito mkuu juu ya njia ya uekeumene, kwa sababu inahusu changamoto ambayo makanisa ya kikristo yanajiandaa kukabiliana pamoja na kujigundua katika mwelekeo wa kiekumene ambao ni wajibu wa pamoja kwa ajili ya utunzaji wa kazi ya uumbaji ya Mungu. Maadhimisho ya kushirikishana katika Kipindi cha uumbaji ni ishara muhimu na hatua ya kuelekea katika muungano kati ya Makanisa. Aidha, ushuhuda huo muhimu umeonekana katika Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko aliomtumia Patriaki wa Kiekumene, Bartolomew I, wa Costantinopol  mnamo mwaka 2017.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.