2018-06-05 13:52:00

Mwili wa Kristo ni taswira ya mwili wa maskini, wadhaifu na wagonjwa!


Kardinali Gualtriero Bassetti Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Italia wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Mwili na damu ya Yesu, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Lorenzo, Perugia nchini Italia, amesema,mwili wa Kristo ni taswira katika kioo cha mwili mwingine kama vile, mwili wa maskini, wa wadhaifu na wagonjwa, hata kama kuna mwili wa Kristo. Amethibitisha hayo tarehe 3 Juni 2018, wakati Mama Kanisa anaadhimisha Sikukuu kubwa ya Mwili na damu ya Yesu (Corpus Domini) mahali ambapo makanisa yote ulimwenguni yamefanya sikukuu hii kwa ukumbusho wa umuhimu wa mwili wake na damu yake Bwana mkombozi wa Dunia, fumbo la Agano jipya na la milele! 

Uwepo wa Yesu hauko mbali kwa kufikiria mbingu, badala yake uwepo ni wa dhati kwa njia ya hija ya mwili ambao  huko karibu na hatua zetu, yupo na sisi, hata katika maisha yetu wakati mwingine yenye kuwa wa usiku wa giza na mwili huo upo katika Ekaristi Takatifu. Kutokana na hilo, wote wamekusanyika na kukaa kwa makini kutafakari Ekaristi iliyo barikiwa. Siku hiyo wote wanataka kukumbuka mkutano wao na Kristo. Ni mkutano mzuri na wenye maana na Yesu wa Ekaristi Takatifu. Aidha Kardinali Bassetti akiwageukia idadi kubwa ya watoto wadogo walio kuwapo kanisani: “Watoto wapendwa, siku ya kupokea Ekaristi Takatifu, daima kukumbuka tukio hilo.

Maneno ya Yesu yanatoa mwelekeo wa kupenda udhaifu wa kila kiumbe. Kwa mfano yule babu ambaye hawezi kuamka tena, ambaye hawezi kuomba tena, hana mtu wa kuongea naye; kwa yule mgonjwa jirani na nyumba ambaye hakuna mtu anaye mtembelea hata siku moja; kwa maskini ambaye wala hakuna anayethubutu kumpatia hata vinsenti. Mungu anatambua kila kiumbe, Mungu anatambua majanga ya watu walio nyanyaswa kijinsia, kihisia, walio uwawa, walioishia katika utupu.

Mungu anatambua kila jina la walio baguliwa, walio achwa peke yao, makumi elfu ya watoto walio uwawa nchini Siria, wakimbizi au wahamiaji ambao wamekufa baharini. Wote hao ni watoto wake na ndugu na kwa upendo wake wanawapasha joto, anawapokea, anawalinda, anawasikiliza na kuwatuliza. Tusisahau kamwe hilo kwa maana uwepo wake ni kweli katika ndugu wadhaifu, ni Kristo mwenyewe, amesisitiza kwa dhati Kardinali Basseti Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Italia.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News
All the contents on this site are copyrighted ©.