2018-06-05 13:34:00

Maandamano ya Ekaristi Takatifu ni mwendo wa Yesu katika umisionari !


Hija ya kitaifa katika madhabahu ya Mama Maria wa Knock nchini Ireland imefanywa na waamini kutoka katika maparokia 56 siku ya tarehe 3 Juni 2018 mahali ambapo Kanisa lilikuwa linaadhimisha Sikukuu ya Mwili na Damu Takatifu ya Yesu Kristo  (Corpus Domini kwa kuongozwa na Askofu Denis Nulty wa jimbo la Kildare na Leighlin nchini Ireland.

Askofu Nulty akiendelea na mahubiri yake amesema, familia moja katika imani imeunganika kwa pamoja ikiwa zimebaki siku 79 kuanza mkutano mkuu wa Familia duniani mjini Dublin. Iwapo Misa siyo takatifu, kuna jambo ambalo labda limekosewa kwa maana Maadhimisho ya misa Takatifu atakayo fanya Baba Mtakatifu labda kwa umati wa watu milioni moja na nusu huko Phoenix Park, mwezi Agosti ujao ni sawa sawa na misa inayoadhimishwa katika mahospitali, nyumba za wagonjwa na wazee, magereza na vituo vyote vya kukaribisha wageni, au misa za kila siku katika maparokia.

Aidha Askofu Nulty akiendelea na mahubiri hayo amesisitiza juu ya maana ya kufanya maandamano, ambayo pia hufanyika kila siku katika madhabahu ya Bikira Maria wa  Knock na kama maandamano yaliyofanyika siku hiyo ya tarehe 3 Juni 2018. Askofu amesema maandamano hayo ni kama mwendo wa kimisionari hivyo, ameshauri kutokuwa vipofu katika hali halisi ya maisha wanayokabiliana nayo  kila siku na ambayo  inakamilishwa katika mchakato wa  sura ya kila mtu kwa maana ni kukutana na sura ya Kristo kama wosia (Gaudete et Exsultate)  wa Baba Mtakatifu Francisko usemavyo na kama  Mama Yetu wa Knock aliyejitokeza mahali pale.

Tendo la kutokea Bikira Maria pale Askofu amethibitisha kwamba, alipendelea ukimya na kusubiri zaidi kwa maana upo utambuzi ya kuwa watu wengi  wanajua kuongea sana, lakini wanatambua uwepo wake na ndiyo maana wako mbele ya madhabahu hayo na mbele ya Yesu wa Ekaristi kujifunua ili  kukutana na Kristo na ambaye anaonekana kwa kila mmoja unaye kutana naye katika hija ya maisha. Askofu Nulty amemalizia akiwatakia wote kuwa na imani kuu kwa maana wanaweza kuona huo uwepo hakika wa Kristo katika maumbo matakatifu ya Ekaristi Takatifu.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.